Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Unyama!! MWANAMKE AJIFUNGUA MTOTO KISHA KUMNYONGA NA KUMZIKA MWENYEWE

MKAZI wa Kijiji cha Kirongaya katika Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, Zainab Abdhalla (25), anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa kosa la kumuua mtoto wake kwa kumnyonga muda mfupi baada ya kumzaa na kumzika mwenyewe.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Koka Moita, ameithibitisha  kutokea kwa tukio hilo lililotokea Juni 5, 2014 saa 11:45 jioni mwaka huu, katika kijiji hicho huku uchunguzi wa awali ukionyesha kuwa mwanamke huyo baada ya kujifungua alikinyonga kichanga hicho kwa kumkaba koo hadi kufa na kisha kumzika nyumbani kwake. 

“Baada ya kujifungua alimnyonga mtoto wake wa kumzaa (mwenye jinsia ya kiume) kwa kumkaba koo hadi kufa na kisha kumzika nyumbani kwake wakati akijua kutenda unyama huo ni kinyume na sheria muda mfupi tu baada ya kumzaa” alisema Moita.

Amesema baada ya Jeshi hilo kupata taarifa ya tukio hilo, maofisa wa Jeshi hilo walifika katika eneo la tukio na kuufukua mwili wa marehemu kisha kuupeleka katika Hospitali ya Usangi, iliyoko Wilayani Mwanga kwa ajili ya uchunguzi zaidi na baadae kuukabidhi mwili huo kwa ndugu na jamaa zake kwa ajili ya shughuli za mazishi.


Kwa mujibu wa Kamanda, Moita, mtuhumiwa huyo tayari anashikiliwa na Jeshi hilo kwa mahojiano na kwamba baada uchunguzi kukamilika atafikishwa Mahakamani kujibu shtaka la kumuua mtoto huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com