Kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka huu watu wanane wamefariki dunia kwa kuumwa na mbwa wenye kichaa katika manispaa ya Songea.
Huku manispaa ya Songea inayotikiswa kwa ugonjwa huo ikiwa haina dawa za kutibu watu walioumwa na mbwa kichaa na pia idara yake ya mifugo haina pesa za mafuta kuzungukia kuua mbwa wenye kichaa.
Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu afisa mifugo wa manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Bw.Gaspar Tillya na kwamba kutoka na hali hiyo msako mkali umekuwa ukiendeshwa wa kuwasaka mbwa wenye kichaa ingawa unakwazwa na ukosefu wa pesa huku wanajeshi wakisaidia kusaka mbwa hao kutokana na baadhi ya mbwa hao kuingia kwenye kambi ya jeshi ya Chandamali ya mjini Songea.
Social Plugin