Basi la supernajimunisa likiwa eneo la tukio leo abiria wakihangaika baada ya ajali hiyo ambayo imejeruhi watu 52 kati 63 waliokuwa ndani ya basi hilo
Abiria wakihangaika baada ya ajali |
Basi likiwa limepinduka
Wimbi la ajali za barabarani limeendelea nchini ambapo leo abiria 63 waliokuwa wanafasafiri kutoka Mwanza kwenda Dar es salaam na basi la Super najimunisa lenye namba za usajili T.242 BRJ wamenusurika kufa baada ya basi hilo kupinduka katika kijiji cha Busanda kata ya Samuye wilaya ya Shinyanga mkoa wa Shinyanga leo majira ya saa tatu asubuhi.
Basi hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina la Dickson Paulo
Majeruhi 52 walikimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya matibabu.
Mganga mkuu wa
mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe ameiambia malunde1 blog kuwa wamepokea majeruhi 52 ambapo kati yao
majeruhi waliolazwa ni 22 na miongoni mwa ambao wanne kati yao hali zao ni mbaya na tayari majeruhi 30 wamesharuhusiwa.
Katika hatua nyingine malunde1 blog imezungumza na majeruhi waliolazwa katika hospitali hiyo ambao wamesema ajali hiyo imetokea baada ya tairi la mbele la basi hilo kupasuka na gari kupinduka mtaroni
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus
Kamugisha alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi wa
awali unaonesha kwamba pamoja na kupasuka kwa tairi basi hilo lilikuwa katika
mwendo kasi.
Kamanda Kamugisha alisema jeshi la polisi
linaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo.
Hata hivyo eneo hilo la Usanda limekuwa sugu kwa matukio ya ajari za barabarani za mara kwa mara na kusababisha vifo vya watu na ulemavu wa kudumu
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog-Shinyanga
Social Plugin