Baada ya kuonekana noti ya shilingi 500 ina na mzunguko mkubwa wa matumizi na inachakaa kwa haraka huku kiwango chake cha kuhimili mizunguko ni miezi sita, Benki kuu ya Tanzania (BOT) inatarajia kubadili noti hiyo na kuifanya sarafu.
Sarafu hiyo ya 500 inatarajiwa kutambulishwa na kuanza kutumika July 2014 ikienda sambamba na kipindi cha mwaka huu wa fedha ambapo unaambiwa hii sarafu ikishatoka inatarajiwa kudumu kwenye mzunguko kwa zaidi ya miaka 20 na kubaki na ubora wake uleule, yani ni imara kuliko noti.
“Tunafanya hivi kwasababu noti ya 500 inachakaa haraka kulinganisha na mzunguko wake na kuwafikia watu wengi pia huchakaa haraka kutokana na mzunguko wa kushikwa na watu wanaofikia mpaka milioni moja kwa siku, hiyo ni idadi kubwa kuliko ya wanaoshika noti ya elfu 10 kwa siku.
via_tza
Social Plugin