Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BAADA YA KUONEKANA KUCHOKA MAPEMA-SASA NOTI YA 500 KUWA SARAFU

500 2
Baada ya kuonekana noti ya shilingi 500 ina na mzunguko mkubwa wa matumizi na inachakaa kwa haraka huku kiwango chake cha kuhimili mizunguko ni miezi sita, Benki kuu ya Tanzania (BOT) inatarajia kubadili noti hiyo na kuifanya sarafu.
Sarafu hiyo ya 500 inatarajiwa kutambulishwa na kuanza kutumika July 2014 ikienda sambamba na kipindi cha mwaka huu wa fedha ambapo unaambiwa hii sarafu ikishatoka inatarajiwa kudumu kwenye mzunguko kwa zaidi ya miaka 20 na kubaki na ubora wake uleule, yani ni imara kuliko noti.
Afisa mkuu wa benki kitengo cha idara kurugenzi za kibenki Patrick Fata amesema 
“Tunafanya hivi kwasababu noti ya 500 inachakaa haraka kulinganisha na mzunguko wake na kuwafikia watu wengi pia huchakaa haraka kutokana na mzunguko wa kushikwa na watu wanaofikia mpaka milioni moja kwa siku, hiyo ni idadi kubwa kuliko ya wanaoshika noti ya elfu 10 kwa siku.
via_tza

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com