Kuhusu kilichotokea baada ya yule baba mchungaji wa Kanisa la Living World Ministry lililopo Ukonga-Majumba Sita jijini Dar, Michael Semeni kudaiwa kufumaniwa na mke wa mtu ni kwamba kanisa hilo limefungwa.
Habari ya mchungaji huyo iliandikwa na gazeti fulani wiki mbili zilizopita ikiwa na kichwa ‘HEE! BABA MCHUNGAJI!’
Katika habari hiyo ilielezwa kwamba baba mchungaji huyo alikuwa akitaka kuvunja amri ya sita na mke huyo wa mtu baada ya mwanamke huyo kwenda kanisani hapo kupata maombi maalum ya deliverance ili apate mtoto.
Ilidaiwa kwamba mara baada ya waumini au kondoo wake kuona picha na habari ya baba mchungaji huyo gazetini walisusa kwenda kanisani hapo.
Habari zilizonaswa kutoka kanisani hapo kutoka kwa muunini mmoja (jina linahifadhiwa) zilidai kuwa baba mchungaji huyo ameingia mitini na hajulikani alipo.
alisema mmoja wa waumini hao
Social Plugin