VIONGOZI wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mkoani Geita wameitaka Serikali mkoani Geita kuwatafutia maeneo ya kuchimba wachimbaji wadogo wadogo kuliko na kuwaacha wanahangaika kila wanapoenda na kukumbatia wachimbaji wakubwa pekee.
Kauli hiyo imetolewa juzi na Mwenyekiti wa chama hichoAliphonce Mawazo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja nya Soko kuu mjini Geita huku akiwatuhumu viongozi wa mkoani kwa kushirikiana na idara ya madini kwa kutowathamini wachimbaji wadogowadogo jambo ambalo amesema kuwa ni hatari kwa vijana ambao hawana ajira.
Aidha aliongeza licha ya wachimbaji wadogowadogo walipewa maeneo ya kuchimba sehemu ya Lwenge lakini maeneo hayo hayana dhahabu na wachimbaji hao wamekuwa wakiilalamikia serikali kwa nguvu zao zote ili iwatafutie maeneo ambayo wataweza angalau kupata chochote kwa ajili ya kuendesha maisha yao.
Kwa upande wa katibu wa chama hicho Soud Ntanyanga alilaani vitendo vinavyofanywa na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Geita kwa kuwaingilia watendaji katika kutekeleza majukumu yao kwa kisingizio cha kwamba chama tawala lazima kitoe maelekezo katika kutekeleza majukumu yao wakati watendaji haohao wanatekeleza sera za nchi.
Naye diwani wa kata hiyo kupitia chadema Donald Ng'wenesho alilaani kitendo cha mwenyekiti huyo wa CCM mkoa kusimama kwenye jukwaa na kusema ni mwizi na kama ana ushahidi aende mahakamani na si kuropoka kwenye majukwaa ya kisiasa na kujitafutia umaarufu usiokuwa na tija katika maeneo ambayo wananchi wake wana shida za kijamii.
Diwani huyo amewataka wananchi kupuuza maneno ya wanasiasa wengine ambao wamekuwa wakipingana hata na sera za chama chao na watu kama hawa ni wasaliti ndani ya chama na hata serikalini.
Na Valence Robert-Malunde1 blog Geita
Social Plugin