Mwanaume mmoja amejikuta akijikata sehemu ya uume wake katika mgahawa mmoja jijini London uliokuwa umefurika watu wengi waliokuwa wakijipatia huduma ya chakula na vinywaji
Polisi walilazimika kutumia gesi ya kuwasha kumzuia mwanaume huyo wakati walipofika ndani ya mgahawa huo baada ya kupatiwa taarifa juu ya tukio hilo.
Msemaji wa polisi amesema kuwa mwanaume huyo anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 hadi 40 ambapo alipata majeraha wakati akitekeleza kitendo hicho.
Alikimbizwa hospitalini Kusini mwa London ambapo hali yake inaendelea vizuri licha ya kuwa madaktari wa upasuaji wameshindwa kurudisha uume wake ambao tayari aliukata.
Mwanaue huyo alichukua kisu kutoka kwenye jiko la mgahawa na kutekeleza kitendo hicho.
Social Plugin