Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

FUATILIA HAPA KILICHOJIRI LEO WILAYANI BARIADI MKOANI SIMIYU

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi Bahati Magamula akifungua mdahalo uliowashirikisha wadau wa zao hilo,wakulima ,wataalamu wa kilimo kutoka halmashauri mbalimbali na waandishi wa habari,mdahalo ambao umeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na demokrasia na utawala bora vijijini (ADLG) chini ya ufadhili wa jukwaa la mashirika yanayojishughulisha na kilimo ANSAF.

Wadau wa kiimo cha zao la pamba kutoka katika wilaya ya Itilima na Bariadi mkoani Simiyu wakiwa kwenye mdahalo wa kujadili changamoto mbalimbali zinazolikabili zao la pamba mkoa wa Simiyu,ambapo wamezitaka mamlaka zinazohusika na zao hilo kuacha kukaa tu ofisini badala yake waanze kuwatembelea wakulima vijijini ili kubaini changamoto zilizopo likiwemo suala la bei,mbegu na madawa ya kuuwa wadudu waharibifu.

Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu  wakiwa katika ukumbi wa Bariadi motel wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa zote zikilenga kupata ufumbuzi wa changamoto za zao la pamba.

Mkulima wa zao la pamba kutoka kijiji cha Mwamapalala wilaya ya Itilima Kalibashia Jilinde akieleza hasara aliyoipata kutokana na kutumia mbegu za pamba za Quiton ambazo hazikuota na kulazimika kurudia mara tatu lakini pia hakufanikiwa,ameitaka serikali  kufanya utafiti wa kina kujua madhara na faida zake  kabla ya kupeleka kwa wakuima kwani wamechangia kuwadidimiza kiuchumi kutokana na kutumia gharama kubwa bila kupata faida.
Wakulima wa zao la pamba wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa na wawezeshaji katika kupata mbinu mpya , maoni,ushauri na mapendekezo ya kuondoa changamoto zilizopo.
Mdahalo unaendelea
Katibu wa mtandao wa vikundi vya wakulima (MVIWATA) wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu  Zabron Sayi akiwaasa wakulima wenzake kuendelea kulima kilimo cha pamba na aliitaka serikali kupitia wizara husika kuhakikiha inawachukulia hatua watumishi wa ngazi za chini wa idara ya kilimo kutokana na kuwepo uzembe mkubwa wa kutowatembelea wakulima ili kufahamu kero mbalimbali zinazo wakabili badala ya kwenda kukamata wakulima walichanganya pamba na mazao mengine.
Wadau wakiwa kwenye ukumbi wa Bariadi motel kwa ajili ya mdahalo wa kujadili changamoto mbalimbali za zao la pamba ikiwa ni pamoja na bei kuendelea kuwa chini ambayo haina tija kwa mkulima.
Mkulima wa pamba kutoka kijiji cha Mlimani kata ya Zagayu Sele Mayenga ambaye alisema ameamua kuachana na kilimo cha pamba kwa kuwa haoni faida kutokana  na kupanda mbegu za Quiton na kushindwa kuota hivyo kuamua kujikita katika kilimo cha mahindi na alizeti.
Mkurugenzi wa ADLG Jimmy Luhende akiwasiisha mada kwenye mdahalo huo kutokana na utafiti walioufanya katika wilaya nane zinazolima pamba kwa mkoa wa Shinyanga na Simiyu,ambapo walibaini wakulima waliowengi hawana kopi za kilimo cha mkataba walichokubaliana na makampuni wala bei watakayowauzia,pia vijiji havifahamu asilimia 10 inayotokana na pamba wanatakiwa wapate kiasi gani kama kijiji  na ucheleweshaji wa pembejeo za kilimo mbegu na madawa ambayo wakati mwingine yanafika mpaka mwezi march wakati tayari pamba inakuwa imeharibika shambani.
Waandishi wa habari wakifuatilia mdahalo uliokuwa ukiendelea.
Wadau wa kilimo  cha pamba mkoa wa Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja.

 Wadau hao waliainisha changamoto mbalimbali ambazo zinachangia zao  la pamba kuendelea kutokuwa na ubora hivyo kukosa thamani kuwa ni pamoja na baadhi ya wakulima kuweka mchanga,sukari,chumvichumvi na maji ili kuongeza uzito kufidia kilo zinazoibwa kwenye mizani ya pamba. wakati wa kuuza kwa mawakala wa kampuni za kununua zao hilo.


picha zote kwa hisani ya Stella blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com