Ndege ndogo ikiwa imebeba wafanyakazi wa jeshi la Marekani imetua kwa dhalura katikati ya barabara nchini Uganda baada ya kuishiwa mafuta.
Philip Mukasa msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda amesema ndege hiyo iliyokua imebeba abiria wanane wakiwemo wafanyakazi wawili wa ndege hiyo, ilikuwa iliyokua ikielekea Sudani ya Kusini baada ya rubani kugundua hakuwa na mafuta ya kutosha aliamua kurudi uwanja wa kimataifa wa Entebbe ndipo ikabidi itue kwa dhalura katikati ya barabara kwenye mji wa Mityana uliopo kilomita 67 (maili 41) kutoka mji mkuu wa Kampala.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa, rubani ametua ndege kwa dhalura katikati ya barabara na watu wote wametoka salama.
Haikujulikana ni kwa nini rubani hakuelekea Sudan ya Kusini na badala yake kaamua kutua katikati ya barabara baada ya ndege hiyo kuishiwa mafuta.
Social Plugin