Kampuni ya teknolojia ya LG imetangaza kuwa itatengeneza TV zenye wembamba wa karatasi, na ambazo unaweza pia kuziviringisha.
Kampuni hiyo imesema ina uhakika wa kutengeneza TV hiyo kwa ukubwa wa inchi 60 (sentimia 152) yenye uwezo wa picha za 'Ultra HD' ifikapo mwaka 2017.
LG ilionesha moja ya TV zake za kwanza zinazoweza kukunjwa katika maonesho ya vifaa vya elektroniki mapema mwaka huu.
Wataalam wanasema TV zinazoweza kujikunja au kuviringishwa zinaweza kutumika kutekeleza ubunifu zaidi.
Social Plugin