Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Hot News!! MAJAMBAZI YAPIGA RISASI BASI LA MAGEREZA KISHA KUPORA MAHABUSU MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM



 Wananchi wakiliangalia basi la mahabusu la Jeshi la Magereza namba MT 0046,  ambalo lilishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana na kudaiwa kumpora mahabusu mmoja na kutokomea naye leo katika Barabara ya Old Bagamoyo,  karibu na Mayfair, Mikocheni, Dar es Salaam. Mahabusu wawili walijeruhiwa na askari mmoja wa magereza. 

 sehemu ya nyuma ya basi hilo ikiwa wazi baada kioo kusambaratishwa na kufanikiwa kumpitishia mwenzao









PICHA NA WADAU WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Basi la Magereza lililokuwa limebeba wafungwa/maabusu limeshambuliwa kwa risasi na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi leo (July 2) katika eneo la Mikocheni, Dar es Salaam.Akizungumza leo, Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camellius Wambura amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa jeshi la polisi limeanza kufanya uchunguzi.Kamanda Wambura amesema ni mapema kutaja nia ya watu hao wenye silaha waliovamia gari hilo kwa kuwa wanaweza kuwa na nia tofauti kabisa na fikra za haraka.

Tunafanya uchunguzi ambao utatufikisha mahali tuweze kubaini ni nini. Inawezekana pengine kuna wahalifu walikuwa katika harakati za uhalifu ghafla wakaona basi lile ambalo lina askari wazuri wenye silaha wakaanza kulishambulia…inawezekana. Au inawezekana vingine vyovyote ambavyo hatuwezi kufikiri wala kubaini.” Kamanda Wambura ameiambia 100.5 Times Fm.
Ameeleza kuwa hakuna maabusu yoyote aliyeweza kutoroka katika tukio hilo na kwamba madhara yaliyotokea kwenye gari hilo sio makubwa. Amesema bado hajapata taarifa yoyote ya uharibifu wa mali au upotevu wa mali uliotokea katika eneo hilo kufuatia tukio hilo.
Akizungumzia watu waliojeruhiwa katika tukio hilo, Kamanda Wambura amewataja watatu waliopata majeraha kuwa ni dereva wa basi hilo, mahabusu mmoja na askari mmoja wa kike.
Kuna baadhi wana michubuko, wale wawili ambao ni dereva na mahabusu mmoja. Lakini kuna askari wa kike ambaye yeye ana majeraha kwenye kifua upande wa kulia. Lakini ni nini kimesababishia michubuko ile hatuwezi kujua kama ni vioo ama ni purukushanai wamejichubua mle ndani au vitu gani.” Amefafanua.
Chanzo:  100.5 Times Fm

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com