|
Hapa ni katika ukumbi wa Kapaya mjini Kahama mkoani Shinyanga ambako leo kumefanyika mkutano mkubwa wa Fursa "Tufanikiwe pamoja"ulioandaliwa na kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya African Barrick inayomiliki migodi ya Buzwagi na Bulyankulu wilayani Kahama kwa kushirikiana na Clouds Media Groups na kukutanisha makundi mbalimbali ya wananchi wakiwemo wasanii,wajasiriamali,wakulima,wafugaji na vikundi vya wadau wa maendeleo.Lengo kuu ni kuwaelimisha na kuwahamasisha wakazi wa Kahama kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo Kahama ambazo zinaweza kuwapatia kipato ama kunyanyua vipato vyao.Mgeni rasmi katika huo mkutano huo alikuwa mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida ndugu Yahaya Nawanda
|
Kulia ni Afisa Mahusiano mgodi wa Buzwagi bi Dorothy Bikurakule kushoto kwake ni mwandishi wa habari gazeti la Habari leo bwana Raymond Mihayo
|
Awali mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group bwana Ruge Mutahaba akizungumza katika mkutano wa Fursa mjini Kahama leo ambapo alisema Tanzania ina rasilimali nyingi na mji wa Kahama unazo fursa nyingi na unaendelea kwa kasi hivyo vijana wanapaswa kuzichangamkia ili kujiendeleza huku akiwataka kutokata tamaa,kujiamini na kuwa na mawazo ya mafanikio siku zote. |
|
Mbele kulia ni afisa mahusiano mgodi wa dhahabu wa Buzwagi bi Blandina Munghezi akifuatilia kilichokuwa kinajiri katika mkutano wa fursa "Tufanikiwe pamoja" mjini Kahama leo |
|
Wakazi wa Kahama wakimsikiliza kwa makini mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group bwana Ruge Mutahaba ambaye alisema chochote kinachoizunguka jamii ni fursa kwa mtu mwenye nia ya kupenda maendeleo na kwamba hakuna haja ya kutafuta kitu kipya katika eneo linalokuzunguka bali ni kuangalia namna ya kuziboresha ili ziweze kuzalisha kipato.Mutahaba aliwataka wananchi kutokata tamaa kwa kukosa mitaji kwani kila kitu kinawezekana kwani hata Clouds Media Groups ilianza kwa mtaji mdogo wakiwa na vyumba viwili pekee na sasa wamefanikiwa kutokana na kutokata tamaa na kuwaza kufanikiwa siku zote.
|
Mgeni rasmi katika mkutano huo wa fursa mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida ndugu Yahaya Nawanda akizungumza na wakazi wa Kahama,ambaye ana mradi wa kuku wilayani kwake,aliwataka wananchi kutobweteka na kukaa vijiweni.
Alisema"Hakuna serikali ambayo itakuletea maendeleo vijiweni,unayesubiri ikuletee pesa,utakaa hadi utachoka,tafuteni fursa katika maeneo yenu,undeni vikundi vya kuwaletea kipato"
Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida ndugu Yahaya Nawanda akizungumza na wakazi wa Kahama leo ambapo pamoja na mambo mengine aliwaasa wakazi wa Kahama kwa wabunifu kwa kuangalia nini kipo katika maeneo ambacho kinaweza kuwaingizia kipato
|
Meneja wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi (unaomilikiwa na African Barrick Gold Mine) ndugu Philbert Rweyemamu akizunguzungumza katika mkutano huo ambapo alisema ABG kwa kushirikiana na Clouds Media Groups wameungana pamoja na kukusanya wakazi wa Kahama hususani vijana ili kuwaeleza kuhusu fursa zinazowazunguka.Rweyemamu alisema fursa inaanza pale mtu anapotambua kuwa kuna fursa hivyo wakazi wa Kahama waangalie katika mazingira yao nini kinahitajika ambacho kinaweza kuwaingizia kipato |
|
Mkutano unaendelea |
|
Meneja wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi Philbert Rweyemamu alisema nchi jirani za Uganda na Kenya zinazidi kuendelea kutokana na kwamba wao wanachangamkia fursa hivyo kuwataka watanzania kuthubutu kuleta mapinduzi badala ya kuendelea kulalamika kwamba ni maskini wakati watanzania wanazo akili za kuweza kufanya mambo makubwa.Pia alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wakazi wa Kahama kufanya kazi na African Barrick Gold Mine |
|
Wakala wa mabasi katika stendi ya Kahama bwana Abdi Mohamed ambaye ni miongoni mwa wakazi wa Kahama akichangia mawili matatu katika mkutano huo wa fursa ambao umetumika kuwaamsha wakazi wa mji wa Kahama kuchangamkia fursa zilizopo katika mazingira yao
|
Mkutano wa fursa uliondaliwa na kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya African Barrick kwa kushirikiana na Clouds Media Groups umekutanisha mamia ya wakazi wa Kahama
Pichani aliyesimama ni mfanyabiashara na mkulima kutoka Kahama akiuliza swali wakati wa mkutano huo wa Fursa mjini Kahama mkoani Shinyanga
Afisa Mahusiano mgodi wa Buzwagi bi Dorothy Bikurakule akizungumza katika mkutano wa Fursa "Tufanikiwe pamoja" ambapo aliwataka wakazi wa Kahama kujiamini huku akiwakaribisha kufanya kazi na African Barrick kwani fursa kwa wananchi ziko nyingi hivyo wajitokeze
|
Mkutano wa fursa unaendelea ambapo wakazi wa Kahama wameelimishwa na kuhamasishwa kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo Kahama ambazo zinaweza kuwapatia kipato ama kunyanyua vipato vyao na kuondokana na umaskini katika jamii. |
|
Mjasiriamali anayejishughulisha na usindikaji wa alizeti akizungumza katika mkutano wa fursa leo mjini Kahama |
|
Kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group bwana Ruge Mutahaba akiwa na msanii wa Movie Bad Boy,ambaye anajishughulisha na uandishi,uigizaji,uongozaji na uzalishaji wa movie mbalimbali |
|
Msanii wa muziki Mwasiti Almas ambaye yuko kwenye fani ya muziki kwa miaka 8 sasa akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka vijana wanaoingia katika fani ya muziki kujituma,kuwa wavumilivu na kuwa na nidhamu katika kazi hiyo kwani ni kama kazi zingine za ofisini |
|
Msanii Mwasiti akiwasisitiza wakazi wa Kahama hususani wanaopenda kazi ya usanii kujitokeza na kuamini kuwa wanaweza lakini waingie kwa kutambua kile wanachokifanya |
Msanii wa bongo fleva Joslin Abraham kutoka Kahama akichana mistari leo katika mkutano wa fursa ulioandaliwa na Clouds Media Groups na African Barrick Gold Mine
Kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba,kulia kwake ni msanii wa bongo fleva Joslin Abraham kutoka Kahama ambaye alichana mistari katika mkutano huo.Kijana huyo alionesha uwezo wake mkubwa katika muziki pamoja na kwamba bado hajatoka.Mutahaba alitumia fursa hiyo kumtaka msanii huyo kujitofautisha na wasanii wengine ili kufikia malengo yake
|
Pichani ni bi Seven Mosha msimamizi wa vipaji Afrika( PAN-AFRICA) ambapo alisema ukitaka kuingia katika kitengo flani unapaswa kuelewa mambo mengi kuhusu kitengo hicho hali ambayo itakuwezesha kutengeneza pesa vizuri |
|
Seven Mosha aliwaasa wakazi wa Kahama kuamini kuwa kila kitu kinawezekana endapo mtu ataweka jitihada za maksudi kufanikisha kile anachokifanyia kazi
Katika mkutano huo wa fursa wakazi wa Kahama waliohudhuria walikaa katika vikundi mbalimbali kisha kujadili namna ya kutumia fursa zilizopo Kahama ili kujiinua kiuchumi
Picha zote na Kadama Malunde -Malunde1 blog
|
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin