Kali ya mwaka!! MWANAMKE AKAMATWA NA POLISI,BAADA YA KUMLAZIMISHA MWANAMME AFANYE NAYE MAPENZI
Sunday, July 06, 2014
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 52 anatuhumiwa kumtishia kwa kisu mwanaume mwenye umri wa miaka 25, baada ya mwanaume huyo kukataa kufanya naye tendo la ndoa. Mwanamke huyo Elizabeth Highley alikuwa anakunywa wine nyumbani kwake pamoja na mwanaume huyo Crue Finley katika eneo la Jensen Beach, mjini Florida, Marekani ambapo mwanaume huyo alikataa kufanya kitendo hicho. Bwana Finley amewaambia polisi kuwa mwanamke huyo alichukua kisu na kuanza kumfukuza nje ya nyumba hadi mitaani. Bwana huyo aliomba msaada baada ya kuona polisi nje ya duka moja. Mwanamke huyo amekamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya kushambulia mtu.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin