Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KIJANA AKUTWA AMEJIUA KITANDANI MKOANI GEITA


  
Mwili wa kijana Paschal Jumbe ukiwa kitandani baada ya kujiua       
          
Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Paschal Jumbe (35) mkazi wa mtaa wa Mission katika kata ya Kalangalala wilaya ya Geita mkoani Geita amekutwa amekufa katika nyumba anayoishi  kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni msongo wa mawazo.

Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa mtaa huo Juma Kajala amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo  saa 2.30 asubuhi  alipigiwa simu na watu wanaoishi naye kwenye nyumba hiyo.

Amesema  baada ya kufika hapo alikuta dirisha  likiwa limefunguliwa na marehemu akiwa amelala kitandani ndipo alipiga simu polisi na walipofika polisi walivunja mlango na kumkuta akiwa amekufa .

Naye dada wa marehemu Nyanyama Jumbe alisema kuwa mdogo wake alikuwa na ugonvi  wa kifamilia na mke wake Reticia Jumbe ambaye walipogombana alikwenda kuishi eneo la Nyankumbu nje kidogo ya mji na huenda ndicho chanzo cha mdogo wake kujinyonga.

Kamanda wa polisi mkoani hapaJoseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio na kwamba uchunguzi zaidi kuhus tukio hilo unaendelea

Na Valence Robert-Malunde1 blog-Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com