Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KIJANA AMBAKA KISHA KUMUUA MAMA YAKE MZAZI,KISA KWANINI MAMA KAPIKA MAGIMBI BADALA YA UGALI


MTU anayedhaniwa kuwa ni mgonjwa wa akili, amembaka na kumuua kwa kumpiga fimbo kichwani na usoni kisha kumnyonga shingo mama yake mzazi mwenye miaka 73, mkazi wa Kijiji cha Ibungila wilayani Rungwe, mkoani Mbeya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alimtaja mtuhumiwa kuwa ni Kiswigo Anganisye (33), mkazi wa kijiji hicho.
Alisema kuwa, tukio hilo limetokea juzi, majira ya saa 6:30 usiku, ambako inadaiwa kuwa, kabla ya kuuawa, marehemu pia alibakwa na mtuhumiwa.
Hata hivyo, Kamanda Msangi alisema kuwa, chanzo cha tukio hilo, inadaiwa kuwa ni baada ya marehemu kumpikia mtuhumiwa magimbi badala ya ugali, ndipo alipochukia na kuchukua uamuzi huo na kwamba amekamatwa na anashikiliwa na jeshi hilo.
Na Samwel Ndoni -Mbeya

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com