Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUHUSU KONOKONO 67 WALIOKAMATWA HUKO MAREKANI

Konokono sitini na saba walio hai wamekamatwa na maafisa wa forodha wa Marekani.

Konokono hao ambao hawaruhusiwi kuingizwa Marekani walikamatwa na maafisa wa forodha kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Los Angeles.

Walikuwa wamesafirishwa kutoka Nigeria, wakipelekwa kwa mtu mmoja mjini California, amesema Lee Harty, msemaji wa mamlaka ya forodha.

Konokono hao ni miongoni mwa konokono wakubwa duniani na huweza kukua na kufikia urefu wa sentimita
 20, wamesema maafisa.

Idara ya kilimo ya Marekani imewateketeza konokono hao baada ya kuwakagua, amesema Bi Harty, kwa sababu hubeba wadudu ambao ni hatari kwa binaadam, wakiwemo wadudu wanaosababisha homa ya uti wa mgongo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com