Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mkazi wa Wilaya ya Mwanga, Innocent Mkali (14) kwa tuhuma za kuwalawiti watoto wawili wa familia moja, katika Kata ya Kirua Vunjo, Wilaya Moshi Vijijini, mkoani humo.
Watoto hao wanadaiwa kulawitiwa na mtuhumiwa baada ya mmoja wao kutoka shule na mwingine wakati akienda shule katika nyakati za mchana.
Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Robert Boaz, amethibitisha tukio hilo.
Alisema Julai 8, mwaka huu, majira ya saa 7.00 mchana, watoto, ambao majina yao yamehifadhiwa, akiwamo mmoja mwenye umri wa miaka tisa na mwingine miaka sita walilawitiwa kichakani katika kata hiyo.
Kamanda Boaz alisema mtuhumiwa alifika katika maeneo ya Kirua Vunjo kwa ajili kufanya kazi za kuvuna katika baadhi ya mashamba yaliyopo maeneo ya jirani na tukio lilipotokea.
“Mtuhumiwa huyo aliwaita watoto hao wakiwa wametoka shule na mwingine akiwa anakwenda shule na kuwadanganya kwa kuwahidi atawanunulia kofia na suruali wasije wakasema,” alisema Kamanda Boaz.
via>>mwananchi
Social Plugin