Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUTANA NA MISS SHINYANGA 2014,TAZAMA PICHA ZAKE 10 KATIKA MATUKIO MBALIMBALI

Pichani ni mrembo wa mkoa wa Shinyanga( Redd's Miss Shinyanga 2014) anajulikana kwa jina la Nicole Franklin Sarakikya,mtoto wa tatu katika familia ya kikristo ya watoto wanne. Mrembo wa mkoa wa Shinyanga mwaka 2014,Nicole Franklin Sarakikya aliyekuwa anawakilisha wilaya ya Kishapu katika mashindano ya Miss Shinyanga 2014 aliyezaliwa mwaka 1993 katika hospitali ya  Mwananchi mkoani Mwanza anasema anapenda sana neno la mungu na anaamini kabisa kwamba hatua aliyoifikia ya kuwa Miss wa mkoa wa Shinyanga ni "Baraka za Mungu"
Ni usiku wa kuamkia Jumapili wiki iliyopita Nicole Franklin Sarakikya(katikati) alitangazwa mshindi katika shindano la Redd's Miss Shinyanga mwaka 2014 lililoandaliwa na Asela Promotions,lililofanyika katika ukumbi wa NSSF mjini Kahama akiwa ni miongoni mwa washiriki 20 kutoka maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga
Nicole Franklin Sarakikya akiwa jukwaani siku ya Shindano la kutafuta mrembo wa mkoa wa Shinyanga mjini Kahama
Mbali na kuwa mrembo,Nicole ana kipaji cha Kuimba,katika shindano la kutafuta mrembo mwenye kipaji mkoa wa Shinyanga (Miss talent Shinyanga 2014) lililofanyika Juni 25,2014 mjini Shinyanga alibahatika kuingia katika warembo watano wenye vipaji.Pichani yuko Jukwaani  mjini Kahama anaonesha kipaji chake cha kuimba wakati wa mashindano ya Miss Shinyanga
Hapa ilikuwa ni katika shindano la kutafuta mrembo mwenye kipaji lililofanyika mjini Shinyanga ambako Nicole Franklin Sarakikya( wa pili kutoka kulia) aliingia katika Top 5.Mrembo wa mkoa wa Shinyanga mwenye kipaji aliyetangazwa kwa mara ya mwisho mjini Kahama alikuwa Irene Makwaiya( wa kwanza kushoto) ambaye naye alikuwa anawakilisha wilaya ya Kishapu
Baada ya kutangazwa mshindi wa taji la Miss Shinyanga,Nicole Franklyn Sarakikya( wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na washindi namba 2,na 3 pamoja na majaji waliotangaza matokeo ya shindano hilo lililolkuwa linajumuisha warembo 20 kutoka maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga


Kabla ya Shindano la Miss Shinyanga warembo 20 waliokuwa wanashiriki shindano hilo wakiongozwa na mkurugenzi wa Asela Promotions bi Asela Magaka( mwandaaji wa Mashindano hayo) walitembelea kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhangija mjini Shinyanga.Katikati ni Miss Shinyanga 2014 Nicole Franklyn Sarakikya akiwa na watoto wenye ulemavu,kushoto ni mshindi wa tatu Rachel Judica aliyekuwa anawakilisha wilaya ya Shinyanga vijijini katika shindano la miss Shinyanga 2014

Kabla ya shindano la Miss Shinyanga 2014,washiriki wakiwa katika maandalizi nje ya Diamond Fields Hotel mjini Shinyanga.Wa pili kutoka kushoto ni Miss Shinyanga 2014 Nicole Franklyn Sarakikya

Kabla ya shindano la Miss Shinyanga 2014- Warembo 20 wakiwa katika picha ya pamoja,mbele wa pili kulia ni miss Shinyanga 2014 Nicole Sarakikya

Kabla ya shindano- washiriki wa shindano la Miss Shinyanga 2014 wakiwa katika pozi,mbele wa tatu kutoka kulia ni Nicole Franklyn Sarakikya.
Akiongea na Malunde1 blog muda mfupi baada ya shindano la Miss Shinyanga kuisha Nicole Franklyn Sarakikya alisema.....

"Nimejisikia faraja, kikubwa namshukuru mungu,mungu kafanya njia,nawashukuru wote walionipa sapoti,walionitia moyo mpaka kufikia hatua hii,nilishindana Miss Kishapu 2014 nikawa namba 1,najivunia kujiamini kwangu,naamini kitu ninachokifanya hata nikisimama mbele za watu nasimama nikiwa najua ninachokifanya kiko sahihi".
Malunde1 blog haikuishia hapo ilitaka pia kujua historia fupi ya mrembo huyu,ndipo akasema....

"Nimezaliwa mwaka 1993, ni mtoto wa tatu katika familia ya watoto wanne,shule ya msingi nilisoma pale shule ya msingi Nyakahoja jijini Mwanza,kidato kwanza hadi cha nne nimesoma New Hellens na baadaye masomo ya ngazi ya Advance nilimalizia Edmund Rice na hivi sasa mimi ni mwanafunzi wa chuo cha Diplomasia nasoma  International relations,napendelea kuimba,kusikiliza na kusoma habari mbalimbali,lakini zaidi napenda kujifunza neno la Mungu maana naamini hata mpaka kufikia nafasi hii ni baraka za mungu"


Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com