Mkoa wa Shinyanga mbali na kuwa na utajiri wa madini ya dhahabu na almasi lakini kuna mambo kadha wa kadha yaliyopo pengine huyajui na ukiyasikia unaweza usiamini.
Mwandishi wa Malunde1 blog
Faustine Kasala anayepatikana kupitia namba 0762 935183 ametembelea wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na kuona maajabu ya jiwe hili linalodaiwa kusikia shida za wananchi.
Mwandishi wa Malunde1 blog
Faustine Kasala anayepatikana kupitia namba 0762 935183 ametembelea wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na kuona maajabu ya jiwe hili linalodaiwa kusikia shida za wananchi.
Unayemuona pichani ni Chifu Makwaia wa Utemi wa Usia akiweka sadaka yake kwenye jiwe la Mwanzuli lililopo Kishapu mkoani Shinyanga linaloaminiwa na jamii kuwa linajibu maswali ya watu wanaofika hapo na kuuliza shida zao. Inaelezwa kuwa mtu ukifika katika jiwe hilo la ajabu kwanza unaanza unaliita jina lake,lina jina jiwe hili " then unasema mimi fulani(taja jina lako) nimekuja kuuliza je! nina UKIMWI?" likitikisika ujue imekula kwako, au katika mishe mishe zangu leo,je nitapata pesa? likitikisika ujue kweli utapata lisipotikisika ujue hutapata kitu.
Ni hayo tu kwa leo tutaelendelea kuwaletea maajabu mbalimbali yanayopatikana mkoani Shinyanga endelea kutembelea Malunde1 blog,Fahari ya Shinyanga
Social Plugin