Nesi wa kituo cha afya cha Katoro wilaya
Geita mkoani Geita, Leah Mganga( 33) mkazi wa katoro, anashikiliwa na
jeshi la polisi kwa tuhuma za mauaji ya kichanga.
Tukio hilo la kushangaza limetokea jana
majira ya saa tisa usiku, wakati mama mmoja aitwaye Mariam Gekera
(23) mkazi wa Nyarugusu, alipofikishwa katika kituo hicho kwa ajili kujifungua
na kisha kupokelewa na nesi huyo ambaye
alikuwa zamu kwa ajili ya kumhudumia.
Akizungumza na waandishi wa habari kituoni
hapo huku akibubujikwa na machozi mzazi huyo alisema kuwa pamoja na
kupokelewa na nesi huyo na kupimwa na kuambiwa mimba imefikia kuzaliwa lakini
huduma za kumsaidia ili ajifungue salama zilianza kusuasua .
Mama huyo alisema alifanikiwa kujifungua japo
kwa shida yeye mwenyewe mtoto akiwa mzima na analia, lakini kwa bahati mbaya
damu zilimrukia nesi huyo kitendo ambacho kilimkera nesi na kuanza kutoa matusi
kwa mzazi huyo.
Kufuatia hali hiyo nesi alikwenda kubadilisha vazi na kurudi na kubeba kichanga na
kuondoka nacho huku mzazi akiuliza mtoto anapelekwa wapi.
“Muda
mfupi nesi alirudi akiwa amekibeba kichanga hicho kwa mikono miwili na kusema “kichanga chako ni kilo tatu na ni kivulana
lakini kimekufa”.alisema mama huyo
Kufuatia tukio hilo malunde1 blog haikukaa
kimya,iliamua kumfuata nesi Leah Mganga ili kujua kulikoni lakini alisema taarifa
zilizotolewa na mzazi huyo si za kweli na kuongeza kuwa yeye alitoa msaada kama
kawaida na baada ya kurukiwa alikwenda kubadilisha vazi jingine na aliporudi
alikuta kichanga kimekufa.
Mganga mfawidhi wa kituo hicho Dk. Alex
Bundala alikiri kuwepo kwa tukio hilo kwenye kikao cha wajumbe wa serikali ya
kijji walichokuwa wamekiitisha mapema asubuhi ya leo kwa ajili ya kuzungumzia
tukio hilo.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Joel Mazemle pamoja na uongozi wake wamelaani
kitendo kilichofanywa na nesi na kuiomba serikali kuchukua hatua kali dhidi ya
mtuhumiwa huyo kwani ni vitendo vingi viovu vinavyofanywa na manesi hao katika
kituo hicho.
Jeshi la polisi mkoani Geita limethibitisha kutokea kwa tukio na kusema
mtuhumiwa anashikiliwa kwa uchunguzi zaidi.
Na Valence Robert-Malunde1 blog-Geita
Social Plugin