Zaidi ya majangili 400 wamekamatwa katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi wakiwa na silaha tano za kivita aina ya SMG na silaha aina ya G3 pamoja na Risasi 357 katika kipindi cha kuanzia june 2013 hadi june 2014
Hayo yalielezwa jana na Mkuu wa Idara ya ulinzi wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi Davis Mushi wakati akitoa taarifa ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya ya Mpanda kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya maji Mjini hapa
Mushi aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo katika kipindi cha mwaka 2013 na 2014 wamefanikiwa kukamata majangili 409 wakiwa na silaha za kivita bunduki aina ya SMG tano ,G3 Bunduki aina ya Riffle nane , Shortgun 21 magobore 138 Bastola mbili na Risasi za SMG 357
Alisema kuwepo kwa makazi ya wakimbizi ya Katumba na Mishamo karibu na Hifadhi kumesababisha wakimbizi wa makazi hayo kujihusisha na shu\ghuli za ujangili kama njia ya kupatia kipato chao
Alifafanua kati ya majangili wanaokamatwa na meno ya tembo baadhi yao huwa ni wakimbizi wanaotoka kwenye makambi hayo ya wakimbizi ya Katumba na Mishamo
Alieleza wakimbizi toka kambi hizo ndio waingizaji wakubwa wa silaha za kivita kama vile Smg , G3 , Sar na Ar 15 ambazo wamekuwa wakizitowa Nchini kwao na kuzitumia kufanyia ujangili ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi
Mushi alieleza uingizaji wa silaha nyingi za kivita smg , G3 na Sar kutoka Kigoma unafanywa na wafanyabiashara haramu wa mano ya Tembo unaofanywa ilikurahisisha shughuli za ujangili
Alisema silaha hizo zinapoingizwa hupewa majangili ili kuwawindia tembo au hudalisha kwa meno ya tembo na silaha hari ambayo inapelekea kuzagaa kwa silaha nyingi za kivita na majangili wengi kwa sasa wamebadilisha matumizi ya silaha kutoka magobore hadi kuwa silaha za kisasa si kwa kuwindia tembo tuu hata wanyama wengine
Alltaja sababu nyingine zinazochangia ujangili katika hifadhi hiyo ni kuwepo kwa mapoli mengi yasiyo na ulinzi hivyo kuwa ni sehemu ya kujifichia kwa majangili na pia wanyama wengi kutoka hifadhi ya Katavi huwindiwa huko mfano ni msitu wa Msaginya
Aidha magobole mengi kumilikiwa kihalali hari hii inafanya watu wengi kumiliki silaha hizo kwani kibali chake ni shilingi elfu moja ambapo kazi kubwa ya Magobole hayo ni ujangili wa wanyama na hasa Tembo
Pia kuwepo kwa silaha zinazomilikiwa na watu kihalali kama vile bundu za aina ya Rifle watu hao wanamiliki silaha hizo wamekuwa wakizikodisha kwa majangili wa wanyama na hasa Tembo
Vilevile kuanzishwa kwa kwa vijiji kando kando ya Hifadhi na hasa ndani ya mita 500 toka mpakani mwa hifadhi kinyume cha sheria ya wanyama pori ya mwaka 2002 hali hii inapelekea baadhi ya waalifu kuhamia kwenye vijiji hivyo na kuendesha shughuli za ujangili ndani ya Hifadhi ya Katavi
Na Walter Mguluchuma -Mpanda Katavi
Social Plugin