JESHI la Polisi Mkoani Dodoma linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Hombolo Justus Jackson (28) kwa tuhuma ya kumuua mwalimu mwenzie kwa kukataa kulipa sh. 1,000 ya bili ya umeme aliyo takiwa kuchangia marehemu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, David Missime amemtaja mwalimu aliyeuawa kuwa ni Fredy Ndahani (29) mwalimu wa shule ya Hombolo.
Misime amesema walimu hao wote wawili walikuwa wakiishi katika nyumba moja na walikuwa wakichangia bili ya umeme katika nyumba hiyo.
Amesema katika mabishano walimu hao waliingia katika ugomvi na hivyo Fredy alisukumwa katika ukuta na kupoteza maisha papo hapo.
Kwa mujibu wa Misime Mtuhumiwa huyo ameshakamatwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika kwa upelelezi.
Social Plugin