Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MASKINI KANYE WEST AZOMEWA NA MASHABIKI JUKWAANI

Video: Kanye West azomewa jukwaani katika tamasha la Wireless, wengine waondoka
Umati mkubwa wa watu walioingia katika tamasha la Wireless huko Finsbury Park, London July 4 walishindwa kumkopesha heshima rapper Kanye West baada ya kusahau kilichompeleka jukwaani hapo na kuanza kutoa hotuba ndefu kama mwanasiasa.
Kanye West aliyekuwa amevaa Mask usoni alijikuta akizomewa kwa nguvu zote na mashabiki hao baada ya kutumia dakika 30 kutoa hotuba akilalamikia makampuni ya mitindo kama Nike na Gucci kuwa yanambagua kwa kuwa yeye ni mtu mweusi.
“Sitataja jina lolote lakini…Nike, Louis Vuitton na Gucci. Msinifanyie ubaguzi kwa sababu mimi ni mtu mweusi ninaefanya muziki.” Alisema Kanye West kwenye maelezo yake.
“Hivi ndivyo ninavyomaanisha…wanasema, ‘Sijui Kanye West ana tatizo gani’ na kuifanya isikike kama mimi ni mtu mbaya katika hali Fulani. Nini nilichowahi kufanya kilichokuwa kibaya zaidi ya kujiamini?” Ni sehemu ya hotuba ya Baba North West.
Malalamiko ya Kanye West yaliwaboa mashabiki ambao mwisho walimkumbusha alichotakiwa kufanya kwa kumzomea huku wengine wakindoka katika tamasha hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com