Mama wa mtoto huyo Rhoda Idetemya akiwa katika kituo cha polisi Kahama baada ya kukamatwa.
Kisima alichotupwa mtoto huyo
Majirani wakiwa katika nyumba aliyokuwa anaishi mama wa mtoto huyo
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake |
Mtoto wa kike mwenye umri wa miezi miwili amekutwa amefariki dunia baada ya kunyongwa na kutumbukizwa na mama yake mzazi katika kisima kilichopo mtaa wa Nyasubi wilayani Kahama katika Mkoa wa Shinyanga.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha tukio hilo limetokea jana ambapo mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Rhoda Idetemya(18) mkazi wa mtaa wa Nyasubi wilaya ya Kahama alimuua kwa kumnyonga shingo mtoto wake huyo kisha mwili wake kuutumbukiza kwenye kisima cha maji ya kunywa.
Mtoto aliyeuawa kinyama amejulikana kwa jina la Elizabeth Idetemya.
Kamanda Kamugisha amewaambia waandishi wa habari (ikiwemo malunde1 blog)waliofika ofisini kwake kuwa ,mwili wa mtoto huyo uligundulika wakati mwanamke mmoja aiitwaye Ada Patrick (25) alipokuwa akichota maji kwenye kisima hicho.
Hata hivyo mtuhumiwa wa mauaji hayo ya kinyama alikamatwa na jeshi la polisi akiwa ndani ya gari wakati akijaribu kutoroka kwenda wilaya ya Bukombe mkoa wa Geita ili kukwepa mkono wa sheria.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
Social Plugin