Kipigo cha mbwa mwizi: Scolari akizungumza na wachezaji wake baada ya kufungwa mabao 7-1 na Ujerumani.
Jukwaani nako hali ilikuwa mbaya sana
Hakuna kwa kujificha: Marcelo baada ya dakika 90 kumalizika.
Pole kaka!: Miroslav Klose, aliyefunga bao la pili akimtia moyo Luis Gustavo
Raha: Toni Kroos alifunga bao la tatu na la nne usiku huu.
Tano hizo: Sami Khedira akifunga bao la tano kabla ya nusu saa
Mabeki wa Brazil walicheza maboya sana
Mmaliziaji: Andre Schurle, alifunga mabao mawili ya mwisho ya Ujerumani, huku mchezaji mwenzake wa Chelsea Oscar akifunga la kufutia machozi.
Kijana umenizingua na uzee huu!: Scolari akizungumza na kocha wa Ujerumani, Joachim Low
Mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuduwazwa na Ujerumani ambao walikuwa mbele kwa mabao 5-0 hadi kufikia dakika ya 29 kipindi cha kwanza.
"Walikuwa bora zaidi yetu," amesema Luiz, ambaye alikuwa nahodha wa Brazil baada ya Thiago Silva kuwa nje. "Ni siku mbaya lakini ni siku ambayo tunatakiwa kujifunza.
"Tunaomba radhi kwa Wabrazil wote. Nilitaka kuwaona wakitabasamu."
Mlinda mlango wa Brazil Julio Cesar ameeleza kwamba kupoteza kwa mchezo huo ni "dhahama."
Mlinda mlango wa zamani wa QPR, 34 amesema: "Ilikuwa vizuri hadi hapa.
"Nawashukuru watu wa Brazil, na mashabiki wanatakiwa kupongezwa kwa ushirikiano wao.
"Wachezaji wanaomba radhi, lakini Ujerumani walikuwa imara, na walilifahamu hilo."
Nahodha wa Brazil David Luiz ameomba radhi kwa Wabrazil baada ya waandaaji hao kuchakazwa kipigo cha aibu cha 7-1 na Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali.

Social Plugin