Ikiwa inakaribia miezi miwili tangu kifo cha msanii wa filamu Bongo, Rachel Leo Haule, vitu vya kutisha vinavyoashiria mambo ya uchawi vimekutwa juu ya kaburi lake, Kinondoni jijini Dar.
Tukio hilo la kustaajabisha, lilidaiwa kutokea Alhamisi iliyopita katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Kwa mujibu wa chanzo chetu, ndugu wa marehemu mmoja ambaye hakujulikana jina walikuwa kwenye makaburi hayo wakifanya kumbukumbu mbalimbali ndipo walipokuta ‘madongoloji’ hayo juu ya kaburi la Recho.
Social Plugin