Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MBUNGE SHIBUDA NOMA,AWACHANA LIVE WASUKUMA,AWATAKA KUACHANA NA DHANA YA "NDUHU TABHU" KWA KILA JAMBO,SIKILIZA HAPA

Mlezi wa chama cha wakulima wa pamba nchini na msemaji wa wabunge wanaotoka katika mikoa inayolima zao la pamba nchini,mbunge wa Maswa Magharibi kupitia Chadema mheshimiwa John Shibuda amewapigia filimbi wasukuma kwa kuwataka kuamka na kueleza wazi wazi matatizo yanayowakabili badala ya kukaa kimya na kusema hakuna tatizo(Nduhu Tabhu” wakati kuna tatizo linawasumbua.

Mheshimiwa Shibuda ameyasema hayo jana mjini Shinyanga wakati wa kongamano la siku moja la wadau wa pamba mjini Shinyanga lililoandaliwa na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania(MVIWATA) na wadau wa pamba kutoka mikoa ya Mara,Simiyu,Geita na Shinyanga.

Kongamano hilo lililenga kujua na kupata ukweli juu ya kile kilichotokea kuhusiana na mbegu mpya ya pamba UK91(zenye kipara) iliyozalishwa na kusambazwa na kampuni ya Quton ambapo mbegu hizo hazikuota vizuri na kuwaletea hasara kubwa wazalishaji wa pamba.

Mheshimiwa Shibuda alisema ni wakati sasa kabila la wasukuma ambao ni wakulima wakuu wa zao la pamba kusema matatizo yanayowakabili hususani katika kilimo cha pamba kwani wamekuwa wakipata hasara na kukaa kimya.

Alisema hapa nchini wasukuma wanafanyiwa dhuluma kutokana na tabia yao ya ukimya yaani Nduhu Tabhu kwa kila jambo hata kama linawaumiza.


SIKILIZA HAPA MHESHIMIWA SHIBUDA AKIWACHANA WASUKUMA NA KUWATAKA KUBADILIKA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com