Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MGAMBO WA KAHAMA WAVUNJA VIBANDA NA KUPIGA HOVYO WAFANYABIASHARA KAHAMA

Mwandishi wa habari hizi Ndalike Sonda akizungumza na wafanyabiashara hao mjini Kahama
Wafanyabiashara wa soko la Mhungula wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wamemuomba Mkuu wa Wilaya hiyo Benson Mpesya Kufika katika soko hilo na kuongea na wafanyabiashara hao ikiwemo kusikiliza kero zao. 

Wafanyabiasha hao wamedai kwamba wamekuwa wakionewa na wanamgambo wa mji wa Kahama kwa kupigwa huku wakidai kuwa wameagizwa na halmashauri kubomoa masoko yasiyokuwa rasmi. 

Mmoja wa wafanyabiashara wa soko hilo Veronika Charles amesema soko hilo lilitengwa na serikali ya kijiji cha Mhungula tangu mwaka 2007 hivyo wanashangazwa na kitendo cha serikali kuagiza migambo kuvunja vibanda bila ya kuwapa taarifa kupitia uongozi wa serikali ya Kijiji.

Mwenyekiti wa soko hilo Jumapili Zacharia amesema wafanyabiashara wa soka hilo wapo kisheria kwani wameshalipia katika serikali ya kijiji na kwamba hizo ni njama za wafanyabiashara wa soko la maila kutaka kuwahamisha. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Inunga Ambapo soko Lilipo Paul Alphonce amesema mgambo hao walipaswa kuambatana na viongozi wa Mtaa husika laikini badala yake wanaingia kinyemela mida ya jioni. 
Ameiomba serikali kufika na kukaa na wafanyabiashara hao pamoja nauongozi ili kujadili mbinu zitakazofuatwa na Wananchi wa Mhungula katika kupata huduma za Kijamii.

Mwandishi a habari hizi amefika katika tukio hio na Kujionea Baadhi ya vibanda vikiwa vimevunjwa huku mwanamke mmoja akiwa ameumia Katika paja lake kwa kupigwa ubao uliokuwa na misumari ambaye amekimbizwa katika hospital ya wilaya ya kahama. 

Hata hivyo wananchi hao wamemtaka mkuu wa wilaya hiyo kufika kusiliza kero zao, pamoja na kuwa jana alitoa agizo la wafanyabiashara wote waliopo katika masoko yasiyo sahihi kuondoka.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com