Mkazi wa Mtaa wa Mhongolo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga John Faustene (46) ameng’oa mabati na Milango ya nyumba yake iliyopo Majengo ambayo wanaishi wapangaji na Mke wake kwa kile kinachodaiwa mke wake Kubeba ujauzito usiokuwa wa kwake.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Noel Mseven, tukio hilo limetokea juzi majira ya saa tano usiku ambapo Faustine alikwenda kwenye nyumba yake na kuanza kufanya kitendo hicho huku wapangaji wasijue la kufanya.
Amesema Faustene alikuwa ameachana na Mke wake huyo aitwaye Anastazia Mtingwa zaidi ya miaka minne ambapo baraza la Kata hiyo lilitoa amri ya Anastazia kuendelea kuishi katika nyumba hiyo huku Faustine akiendelea kutoa matumizi.
Baada ya Anastazia kupata ujauzito ambao inadaiwa ni ya Mwanamume mwingine, Faustine amepeleka mashitaka baraza la Kata ili aondoke katika Nyumba hiyo, na kutoa taarifa kwa wapangaji kuhama katika nyumba hiyo ifikapo Aprili mwaka huu.
Mseven Amesema utaratibu wa kuwahamisha wapangaji ulishindikana na kupewa tena hadi Julai Mwaka huu wawe wamehama, lakini Anastazia aliwaongezea mkataba wa mwaka mmoja ndipo Faustine akaamua kufanya kitendo hicho.
Hata hivyo Faustiene amerudi leo asubuhi katika nyumba hiyo ili kuchukua milango na Mabati, lakini hakufanikiwa baada ya kuwakuta askari polisi ambao wamemkamata na hadi sasa anashikiliwa katika kituo cha polisi wilaya ya Kahama.
Na Ndalike Sonda-Kahama
Social Plugin