Halida Ng’anguli akiwa ameanguka nje ya choo katika uwanja wa Samora kabla ya kufariki dunia
WAKATI waislamu nchini jana wameungana na waislamu wenzao duniani kuswali sala ya Iddi mkoani Iringa swala hiyo imemalizika vibaya kufuatia kifo cha muumini mwenzao Halida Ng’anguli mkai wa Mwangata C ambae ni shangazi wa manahabari wa gazeti la majira Iringa Zuhura zuhkeri kufariki dunia baada ya masaa machache toka aanguke chooni uwanja wa Samora.
Tukio la kuanguka kwa mwanamke huyo lilitokea majira ya saa tatu asubuhi wakati waumini wa dini ya Kiislamu ambao walikuwa wakiswali pamoja katika uwanja wa samora mjini Iringa kumaliza swala na kuanza maandalizi ya kuondoka uwanjani hapo kabla ya mmoja kati ya viongozi kwa kutumia kipasa sauti kutangaza tukio la kuanguka kwa mwanamke huyo huku akiwataka wanawake kwenda eneo la tukio katika vyoo vya wanawake ili kutoa msaada zaidi.
Hata hivyo jitihada za waumini hao wanawake pamoja na askari waliokuwepo uwanjani hapo zilifanikisha kumkimbiza mwanamke huyo hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi.
Mbali ya jitihada kubwa za madaktari wa Hospitali hiyo kutaka kunusuru maisha yake bado hali ilionekana kuwa mbaya zaidi kutoka na tatizo ya ugonjwa wa kisukari lililokuwa likimsumbua .
Yapata majira ya saa 4 usiku mwanamke huyo alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu Hospitalini hapo.
Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho Shangazi wa marehemu mwanahabari Zuhura Zukheri alisema kuwa shangazi yake alifariki majira ya saa 4 akiwa katika matibabu na kuwa toka alipofikishwa Hospitali hapo hali yake ilikuwa mbaya na hakuweza kupata nafuu.
Zuhura alisema kuwa tatizo kubwa lililokuwa likimsumbua ni ugonjwa wa Kisukari na kuwa shughuli za mazishi zimepangwa kufanyika leo ambayo ni siku ya Iddi pili majira ya saa 10 jioni.
Social Plugin