Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWANAMKE AZAMA KWENYE BWAWA AKIMWOKOA MBWA ASIZAME

Mwanamke azama bwawani akijaribu kumuokoa mbwa  aliyetaka kuzama
Mwanamke mweye umri wa miaka 29 aishie Washington,Marekani ameripotiwa kuzama katika bwawa kubwa la kuvulia samaki wakati akijaribu kumuokoa mbwa wake aliyetaka kuzama.
Mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Sabra Crafton, mkazi wa Cashmere, Washington alikutwa na tukio hilo wakati akiwa na rafiki yake wa kiume kando ya bwawa la kuvulia samaki.
Rafiki yake huyo wa kiume alimuambia mkuu wa kituo cha polisi cha Chelan kuwa walikuwa wanamrushia mbwa huyo vitu majini na yeye anavifuata kama mchezo lakini baadaye mbwa huyo alionekana kutaka kuzama na ndipo Sabra Crafton akaamua kuingia kumuokoa.
Hata hivyo hali ilikuwa mbaya kwa kuwa Mwanamke huyo alizidiwa na kuzama yeye na mbwa wake aliweza kutoka.
Afisa wa polisi wa Chelan alieleza kuwa baada ya kupewa taarifa walifika katika eneo la tukio na waliweza kumpata na kumtoa kwenye maji mwanamke huyo na kumpa huduma ya kwanza kwa dakika 30 kabla hawajamkimbiza hospitalini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com