Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SIRI YAFICHUKA KUHUSU KUCHAKAA SANA KWA NOTI YA SHILINGI 500

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema sababu ya noti ya  sh. 500 kuchakaa mapema ni kutokana na kutumika na watu wengi wasio na mzunguko wa huduma za kibenki.

Akizungumza katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba), Ofisa wa BoT, Abdul Dollah, alisema noti zote zinatengenezwa kwa malighafi ya aina moja, lakini kinachotokea ni noti ya sh. 500 kutumika kupita kiasi.
 "Ni asilimia 14 ya Watanzania ndio wanatumia huduma za kibenki, waliosalia hawatumii, sasa ukija katika noti za sh. 500 na 1,000, zinachoka sana maana ndizo zinazoshikwa na watu wengi wa tabaka la kawaida"
alisema.

Aliwataka wale wenye noti zilichokaa kuzirudisha BoT, ili wapatiwe noti mpya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com