Dj Migeto enzi za uhai wake Baada ya mwili wa marehemu Juma Migeto kutolewa ulikokuwa umehifadhiwa tayari kwa safari kutoka Jijini Dar es salaam kuja Shinyanga |
Wakazi wa mkoa wa Shinyanga na nchi kwa ujumla wameshtushwa na taarifa za kifo cha DJ maarufu mkoa wa Shinyanga na nchi kwa ujumla Juma Migeto aliyefariki dunia jana majira ya saa tano asubuhi wakati akipata matibabu katika hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa kaka yake na marehemu bwana Joram Mahugi marehemu Juma Migeto alikuwa ameugua kwa muda mrefu na alikuwa anasumbuliwa na tatizo la kuhara na kutapika damu.
Akizungumza na Malunde1 blog kwa njia ya simu muda mfupi uliopita kaka yake na marehemu, Joram Mahugi amesema mwili wa marehemu Juma Migeto unasafirishwa kutoka Jijini Dar es salaam asubuhi hii kuja Mkoani Shinyanga na mazishi yanatarajia kufanyika kesho Jumatano saa saba mchana katika makaburi ya Majengo mjini Shinyanga.
Hivi sasa msiba wa marehemu Juma Migeto upo nyumbani kwao eneo la Kambarage karibu kabisa na uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
"Mwanzo tulikaa kikao cha familia tukaona ndugu yetu Juma Migeto azikwe hapa Dar es salaam kutokana na gharama pamoja na dini kwani marehemu alikuwa Mwislam,lakini baadaye tulikaa tena tukakubaliana mwili wa marehemu usafirishwe kuja Shinyanga,hivyo sasa tunasafirisha mwili wa marehemu,na marehemu atazikwa Shinyanga",amesema Joram Mahugi.
Juma Migeto,mzaliwa wa Shinyanga alikuwa anajishughulisha na kazi ya U Dj mkoani Shinyanga na baadaye kuhamia jijini Dar es salaam akiendeleza kazi yake ya U dj katika maeneo mbalimbali jijini humo.
Taarifa zaidi utaendelea kuzipata kupitia blog hii ya Malunde1 blog,Fahari ya Shinyanga
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Social Plugin