Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAZAMA PICHA_ HILI NDILO TUKIO KUBWA HUKO TINDE- SHINYANGA MWISHONI MWA WIKI ILIYOPITA

Ni Jumapili ya Julai 13,2014-Waziri wa nchi,ofisi ya rais,mahusiano na uratibu Stephen Wasira akizungumza na waumini wa kanisa la romani katoliki Tinde mkoa wa Shinyanga ,wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa lililopewa jina la Papa John Paul wa II.Kwenye harambee hiyo Wasira alimuwakilisha waziri mkuu Mizengo Pinda ambaye alialikwa kuwa mgeni rasmi,ambapo aliwataka viongozi wa madhehebu ya dini kuendelea kushirikiana na serikali kuliombea taifa liendelee kuwa na amani kwani siri kubwa ya amani ni upendo,mshikamano na umoja wa watanzania.
Jiwe la msingi ambalo limewekwa na Waziri wa nchi,ofisi ya rais mahusiano na uratibu kwaniaba ya waziri mkuu Mizengo Pinda,ambaye alishindwa kufika kutokana na kuwa na majukumu mengine ya serikali.
Wanakwaya wakiimba wakati wa ibaada ya misa kabla ya kuanza harambee.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akizungumza na waumini wa kanisa la romani katoliki pamoja na wageni waalikwa kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa.
Mapadrii wakiendelea na ibada ya misa
Ibada inaendelea
Waziri wa nchi,ofisi ya rais,mahusiano na uratibu Stephen Wasira akiweka jiwe la msingi kwenye jengo la kanisa ambalo linaendelea kujengwa,ambapo Wasira alimuwakilisha waziri mkuu Mizengo Pinda ambaye alialikwa kuwa mgeni rasmi kwenye harambee hiyo.
Viongozi wakielekea eneo linapowekwa jiwe la msingi
Waziri Wasira akiwapongeza viongozi kwa kazi nzuri iliyofanyika.
Waziri wa nchi,ofisi ya rais,mahusiano na uratibu Stephen Wasira akizungumza na waumini wakati wa harambee iliyofanyika mji wa Tinde mkoani Shinyanga,ambapo alimuwakilisha waziri mkuu Mizengo Pinda.

Picha zote kwa hisani ya Stella blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com