TAZAMA PICHA TUKIO ZIMA HITIMISHO LA AFRICAN BARRICK -BUZWAGI BRAZUKA BONANZA,ZAWADI NJE NJE
Sunday, July 13, 2014
Lile Bonanza babu kubwa maarufu kwa jina la "BRAZUKA BONANZA" ambalo limekuwa gumzo mjini Kahama katika siku hizi ambapo michezo ya kombe la dunia inafikia tamati leo nchini Brazili,bonanza ambalo limeandaliwa na kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya African Barrick Gold kupitia mgodi wake wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga leo limefikia tamati.Michezo mbalimbali leo imefanyika katika uwanja wa taifa wa Kahama,michezo hiyo ni pamoja na mpira wa miguu,kukimbiza kuku na mbio za magunia.Zawadi mbalimbali zimetolewa kwa washindi.Lengo la Brazuka Bonanza ni African Barrick kuhamasisha umoja,ushirikiano na umoja katika kuhakikisha kuwa mgodi na jamii zinafanikiwa kwa pamoja
Ilikuwa burudani mwanzo mwisho,pichani watot wa kiume kutoka Kahama wakikimbiza kuku ambapo aliyebahatika kukamata jogoo huyo aliondoka naye kama zawadi ya ushindi huo .Mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Kahama ndugu Benson Mpesya
Kushoto ni Mabula Marco kutoka Majengo mjini Kahama,mtoto ambaye alifanikiwa kukamata kuku,akishikana mkono wa hongera na afisa mahusiano mgodi wa Buzwagi bi Dorothy Bikurakule(kulia)katikati ni makamu mwenyekiti chama cha mpira wa miguu wilaya ya Kahama bwana Tito Okuku Obata.Hayo ndiyo matunda ya ABG-Buzwagi Brazuka Bonanza
Mc kushoto akiwa na mtoto Catherine ambaye pia anatoka Majengo mjini Kahama,mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Majengo ambaye alifanikiwa kukamata kuku wakati wa mchezo wa kufukuza kuku kwa upande wa watoto wa kike
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akikagua timu za Bodaboda fc na Afya fc kabla ya mpambano kusaka mshindi wa kwanza katika Soka Bonanza iliyoanza Julai 10 mwaka huu katika uwanja wa taifa Kahama.Hapa anashikana mikono na waamuzi wa mechi hiyo,nyuma yake ni mkurugenzi wa mji wa Kahama bwana Felix Kimario
Zoezi la kukagua timu linaendelea Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya (aliyeshikilia kipaza sauti) akizungumza baada ya kukagua timu,ambapo pamoja na mambo mengine alipongeza kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold kwa kuwa karibu na wananchi wa Kahama kwani wanaifanya Kahama kwenda na wakati,huku akisifu kampuni hiyo kwa kuwaletea maendeleo wananchi wa Kahama kwani mbali na kuandaa bonanza hilo pia wanatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ujenzi wa barabara za lami,shule nk Kulia ni afisa mawasiliano mgodi wa dhahabi wa Buzwagi bi Blandina Munghezi,kushoto kwake ni bi Kisumbo Marick ambaye ni msaidizi wa meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi wakifuatilia kilichokuwa kinajiri uwanjani katika Brazuka Bonanza iliyoandaliwa na African Barrick Gold Mine
Kijana Festo Mahangaiko kutoka Nyihogo akiwa ameshikilia kuku wake baada ya kufanikiwa kukamata kuku katika uwanja wa taifa Kahama leo jioni
Mbio za kwenye magunia nazo zilikuwepo kwenye Bonanza la Brazuka lililondaliwa na African Barrick Gold kupitia mgodi wake wa Buzwagi Kahama,Mbele ni mshindi katika mbi hizo kijana George Mussa ambaye aliondoka na shilingi elfu kumi kama zawadi yake ya ushindi
Katikati mwenye suti ni mkuu wa wilaya ya Kahama ndugu Benson Mpesya,kulia kwake ni bwana Amos John ambaye ni kaimu meneja mkuu mgodi wa Buzwagi,akifuatiwa na afisa mahusiano mgodi wa Buzwagi bi Dorothy Bikurakule(tisheti nyekundu),wa kwanza kulia ni bwana Sweetbert Mapolu ambaye ni afisa mwajiri mfawidhi mgodi wa Buzwagi.Wa pili kutoka kushoto ni makamu mwenyekiti chama cha mpira wa miguu wilaya ya Kahama bwana Tito Okuku Obata,kulia kwake ni afisa habari utamaduni na michezo mji Kahama bwana Julius Masubo Kambarage,akifuatiwa na mkurugenzi wa mji wa Kahama bwana Felix Kimario wakiwa katika uwanja wa taifa Kahama jioni ya leo katika Bonanza lililondaliwa na African Barrick
ABG Buzwagi Brazuka Bonanza ilihitimishwa kwa mechi kali kati ya timu ya Bodaboda Fc na Afya fc(jezi nyeupe) ikiwa ni timu ambazo zimefanikiwa kufika fainali.Mashindano ya mpira wa miguu(SOKA BONANZA)yalianza Julai 10,2014 yakishirikisha timu 8 za Kahama ambazo ni Timba fc,Afya fc,Bodaboda fc,Daladala fc,Stand fc,Bajaji fc,Halmashauri ya mji Kahama fc na Wasanii fc.Na mshindi amepatikana leo fuatilia hapo chini
Wakazi mbalimbali wa Kahama wakifuatilia mechi ya fainali kati ya Bodaboda fc na Afya fc
Tunaangalia mechi ya fainali kati ya Bodaboda fc na Afya fc
Mechi kati ya Bodaboda fc na Afya fc ilikuwa ngumu hadi dakika 90 zinaisha walikuwa sare 2-2,penati zikapigwa bodaboda fc 3,Afya fc 1,hivyo Bodaboda fc kutangazwa washindi katika mechi hiyo na ndiyo washindi wa kwanza,wakifuatiwa na Afya fc huku mshindi wa tatu katika soka Bonanza wakiwa ni Daladala fc
Mashabiki wa Bodaboda fc wakishangilia ushindi baada ya kuwabamiza Afya fc 3-1
Kulia ni afisa mawasiliano mgodi wa dhahabi wa Buzwagi bi Blandina Munghezi,kushoto kwake ni bi Kisumbo Marick ambaye ni msaidizi wa meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi wakiwa katika pozi muda mfupi baada ya mechi kali kati ya Bodaboda fc na Afya fc kuisha
Shangwe baada ya ushindi wa Bodaboda fc zikiendelea jioni ya leo mjini Kahama
Baada ya meshi ya fainali kuisha_ Washindi wa kwanza katika Soka Bonanza Bodaboda fc wakiwa katika mkao wa kula wakisubiri zawadi kutoka African Barrick Gold-Buzwagi
Kulia ni mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akikabidhi pesa taslimu shilingi laki 5 kwa mwakilishi wa Bodaboda fc,ambapo mshindi wa pili Afya Fc walipata shilingi laki 2,mshindi wa tatu Daladala fc wakipata shilingi laki 1.Hata hivyo timu zote zilizoshiriki mashindano hayo zilipewa mpira mmoja kila timu,isipokuwa timu ya Wasanii fc ambayo ilinyimwa mpira kutokana na utovu wa nidhamu baada ya kususia mechi iliyopangwa kuchezwa leo asubuhi dhidi ya Daladala fc,na baada ya kutoonekana uwanjani Daladala fc wakapewa ushindi na kuwa washindi namba 3
Kushoto mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akikabishi zawadi ya shilingi laki 2 kwa mwakilishi wa Afya fc,ambao ni washindi wa pili katika Soka Bonanza.Aidha katika Soka Bonanza mchezaji Obete Pastro kutoka Afya fc alitangazwa kuwa mfungaji bora na kujinyakulia kiasi cha shilingi elfu 50 kama zawadi na golikipa bora alitoka Afya fc pia
Wa pili kutoka kushoto ni kaimu meneja mkuu mgodi wa Buzwagi bwana Amos John akizungumza baada ya Soka Bonanza kuisha na washindi kupewa zawadi.John alisema African Barrick Gold wataendelea kushirikiana na jamii ya Kahama ili kujenga undugu na kuimarisha umoja na mshikamano katika kuhakikisha kuwa jamii ya Kahama na kampuni hiyo wanafanikiwa pamoja,huku akiwaomba wakazi wa Kahama kuendelea kushirikiana na mgodi huo. Usiku huu katika uwanja wa Taifa Kahama burudani inaendelea ambapo msanii Christian Bella na Ney wa Mitego wanatoa burudani kwa wakazi wa Kahama huku mechi ya fainali kombe la dunia kati ya Ujerumani na Argentina zikioneshwa kupitia screen kubwaaa,na tangu kombe la dunia African Barrick Gold-Buzwagi wamekuwepo uwanjani hapo kuwaburudisha wakazi wa Kahama kwa kuonesha mechi zote zinazochezwa nchini Brazil <<BOFYA HAPA KUONA BURUDANI INAYOENDELEA MJINI KAHAMA,NEY WA MITEGO NA CHRISTIAN BELLA>>
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin