Sehemu ya baadhi ya watu waliojeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu uliotokea jana usiku katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Selian,jijini Arusha kwa matibabu.
Pichani ni Askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ kitengo cha Mabomu wakiwa katika eneo la tukio ambapo bomu lilirushwa ndani ya Mgahawa ujulikanao kwa jina la Traditional Indian Cusine uliopo pembeni ya hotel ya Gymkana jijini Arusha,aidha taarifa za awali zinaeleza kuwa watu nane wamejeruhiwa vibaya na mlipuko huo .
Picha ni majeruhi wa mlipuko wa Bomu uliotokea katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine aliyejulikana kwa jina la Deepak Gupta (25),akiwa amelazwa katika hospitali ya Selian,katika chumba cha watu mahututi (ICU),mara baada ya kukatwa mguu wake mmoja wa kushoto kutokana na mhuu huo kujeruhiwa vibaya na bomu.
Asubuhi ya leo askari Polisi na wa Jeshi wameizingira nyumba ya Serikali ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo iliyopo jirani na Mahakama Kuu Arusha wakijaribu kutegua kinachodhaniwa kuwa bomu kikiwa kimetegwa katika geti la kuingilia nyumba hiyo na watu wasiojilikana.
HatA kinjia kinachokatiza maeneo hayo kutokea Mt Meru Hotel nacho kimefungwa kwa muda.
Wakati huo huo kuna taarifa za usiku zikieleza watu kadhaa wamejeruhiwa katika Mgahawa mmoja maeneo ya Gymkhana Jijini hapa na wawili kati yao wako katika hali mbaya.
Hili litakuwa tukio la sita kutokea katika Jiji la Arusha ndani ya muda mfupi, kuanzia May 2013 mpaka sasa.
Tukio la kwanza lilikuwa Kanisani Olasiti watu watatu wakafa.
Baadee katika Mkutano Chadema Soweto watu watatu wakafa tena na mamia kulemaa
Ikafuata Usa River siku ya Mkesha wa mwaka mpya kwa wamama waliokuwa wanatoka kanisani
Halafu katoka Bar ya Arusha Night Park
Juzi hapa ikawa kwa nyumbani kwa Sheikh maeneo ya Majengo
Na sasa katika hiyo Vama Restaurant na chupuchupu kulipua nyumbani kwa RC!

Social Plugin