Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAZAMA PICHA_AFRICAN BARRICK NA CLOUDS MEDIA GROUP WAKUTANA NA WASANII NA WAJASIRIAMALI MJINI KAHAMA


Wasanii wa maigizo kutoka kundi la Fighters wakiwa katika pozi kwenye mkutano wa Fursa"Tufanikiwe pamoja" ndani ya ukumbi wa Nitech mjini Kahama,mkutano huo ni wa pili kukutanisha wasanii na wajasiriamali mbalimbali wa Kahama uliondaliwa na African Barrick Gold Mine na Clouds Media Group



Ndani ya ukumbi wa Nitech mjini Kahama mkoani Shinyanga ambako kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya African Barrick Gold( inayomiliki migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi wilayani Kahama ) kwa kushirikiana na Clouds Media Group wamekusanya wakazi wa Kahama kuwaelimisha na kuwahamasisha kuchangamkia fursa zilizopo katika mazingira yao.Mkutano wa kwanza ulifanyika jana(Julai 4,2014 mjini Kahama) ulikutanisha pamoja wasanii na wajasiriamali mbalimbali,leo umefanyika mkutano wa pili ambapo wakazi wa Kahama ,kila mmoja alipata fursa ya kutoa wazo lake ambalo anafikiri litamsaidia kujipatia kipato huku waandaaji wa mkutano huo wakitumia fursa hiyo kuwaonesha njia ya mafanikio wakazi wa Kahama.

Kulia ni mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba akiwa na msanii wa bongo fleva Waziri Ally ambaye alionesha kipaji chake cha kuimba.Ruge alisema Clouds Media Group inaangalia namna ya kusaidia wasanii hivyo kuwataka wakazi wa Kahama kuchangamkia fursa zilizopo katika mji wa Kahama unaoendelea kwa kasi,pia wazungumzie mambo mazuri kuhusu Kahama
Pichani ni baadhi ya wasanii wa maigizo kutoka kundi la Fighters wakiwa ukumbini,ni miongoni mwa vikundi vitano vya wasanii kutoka Kahama vilivyojitokeza katika mkutano huo wa Fursa"Tufanikiwe pamoja"
Wasanii wa Maigizo kutoka kundi la Fighters wakiwa katika pozi ndani ya ukumbi Nitesh mjini Kahama leo

Wasanii wa kizazi kipya  Chris John na Tonny John wakifanya yao ukumbini
Mwanamuziki Mwasiti na msimamizi wa vipaji vya wasanii Afrika bi Seven Mosha wakiangalia burudani kutoka kwa vijana wa Kahama
Mkuregenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba akizungumza na wakazi wa Kahama wakiwemo wasanii,wafanyabiashara na wajasiriamali mbalimbali katika ukumbi wa Nitech mjini Kahama.Ruge aliwashauri wasanii kuwa na majina ya vikundi yenye urafiki na biashara kwani kama jina la kikundi halivutii ni vigumu kupata wateja.


Joyce Luleka maarufu kwa jina la "MALAJI LAINI" ambaye anajihusisha na uuzaji wa vyakula vilivyopikwa(Mama Lishe) akizungumza katika mkutano huo kuhusu mambo ya ujasiriamali

Wa pili kutoka kulia ni afisa Mahusiano Mgodi wa Buzwagi(unaolimiliwa na African Barrick) bi Dorothy  Bikurakule,nyuma yake ni mwandishi wa habari kutoka Radio Kahama Paulina Juma  wakiwa katika ukumbi wa Nitech wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini 


Ndani ya ukumbi wa Nitech mjini Kahama wakifuatilia mkutano uliokuwa ukiendelea ulioandaliwa na Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu ya African Barrick  Gold kwa kushirikiana na Clouds Media Group

Kushoto ni mwanamuziki Mwasiti Almas,katikati ni  msimamizi wa vipaji Afrika bi Seven Mosha akifuatiwa na mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba wakiwa katika ukumbi wa Nitech wakishuhudia vipaji vya wasanii kutoka mji wa Kahama mkoani Shinyanga 
 Kundi la wafanyabiashara na wajasiriamali-Kila mmoja alitoa wazo lake na kusikilizwa na wandaaji wa mkutano huo yaani Clouds Media Group na African Barrick Gold Mine
Kundi la wasanii wakijadili mawazo yao-Aliyesimama ni Mwakilishi wa Clouds Media Group bwana Raymond Mtani akizungumza na kundi la wasanii kutoka Kahama ambapo aliwataka wasanii kujitambua na kukumbuka kuwa maisha yanakwenda hatua kwa hatua na kuacha kufikiria kuhusu mambo makubwa kwa wakati mfupi hivyo kuwataka kujituma na kuwa wavumilivu katika kufikia mafanikio wanayoyataka.

Wasanii,wafanyabiashara na wajasiriamali waliokutanishwa na African Barrick Gold Mine na Clouds Media Group watakutana tena Julai 14,2014 mjini Kahama kujua wapi wakazi wa Kahama wamefikia baada ya kuoneshwa fursa zilizopo Kahama kwa ajili ya kupata ama
 kuinua vipato vyao

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog


<<<BOFYA HAPA KUONA KILICHOJIRI MKUTANO WA KWANZA WA ABG NA CMG MJINI KAHAMA>>

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com