|
Hapa ni ndani ya ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,ambako leo kumefanyika mkutano mkuu wa mwaka wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga.Mambo kadha wa kadha yamejadiliwa,lakini pia uchaguzi wa kumpata naibu meya kwa awamu ijayo ya mwaka 2014/2015 umefanyika.Kushoto ni diwani wa viti maalum kupitia CHADEMA bi Zainabu Heri,kulia kwake ni mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA mheshimiwa Rachel Mashishanga wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika mkutano huo/Baraza la madiwani wa manispaa ya Shinyanga yenye kata 17
Aliyesimama ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga(mwaka 2013/2014) ndugu David Nkulila,diwani wa kata ya Ndembezi kupitia ccm akizungumza kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa nafasi ya naibu meya mwaka 2014/2015.Kushoto kwake ni mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga ndugu Gulam Hafeez Mukadam,kulia ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Dkt Anselm Tarimo |
|
Baraza la madiwani linaendelea ndani ya ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo,ambapo uchaguzi kiti cha naibu meya ambaye kisheria kufanyika kila mwaka umefanyika |
|
Waandishi wa habari nao walikuwepo,pichani kila mmoja yuko bize kivyake |
|
Katika baraza hilo la madiwani wa manispaa ya Shinyanga wajumbe wa kamati mbalimbali walitangazwa,kamati hizo ni pamoja na kamati ya miundombinu,uchumi na elimu,Ukimwi,Ajira na kamati ya fedha Kushoto ni mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga bwana Festo Kang'ombe akizungumza jambo na mstahiki meya ndugu Gulam Hafeez Mukadam,wa tatu ni mwenyekiti wa muda wakati wa uchaguzi wa naibu meya ndugu Thomas Chuma Maganga diwani wa kata ya Lubaga kupitia chama cha mapinduzi |
Diwani wa kata ya Kitangiri kupitia CHADEMA ndugu George Mussa Kitalama (aliyeteuliwa na chama kugombea nafasi hiyo)akiomba kura kutoka kwa wajumbe 21 waliotakiwa kupiga kura kuchagua naibu meya wa manispaa ya Shinyanga katika mwaka 2014/2015
|
Kulia ni katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga ndugu Boniface Chambi,kushoto kwake ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Dkt Anselm Tarimo wakifuatilia uchaguzi wa nafasi ya naibu meya |
Diwani wa kata ya Ndembezi kupitia ccm ndugu David Nkulila,ambaye aliteuliwa na ccm kugombea kiti cha naibu meya akitetea kiti chake/akiomba kura kwa wajumbe ili wampatie ridhaa ya kuwa naibu meya tena wa manispaa ya Shinyanga kwa mwaka 2014/2015.Nkulila alikuwa naibu meya mwaka 2013/2014 lakini kutokana na chama chake kumwamini kwa uchapakazi wake wamemteua kuwania kiti hicho katika mwaka 2014/2015
|
Kampeni kutoka kwa wagombea kutoka vyama viwili yaani CCM na CHADEMA zinaendelea.Baraza la madiwani wa manispaa ya Shinyanga linaundwa na madiwani kutoka vyama viwili pekee vya upinzani |
|
Ndani ya ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo madiwani wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea |
|
Zoezi la kukusanya kura linaendelea,afisa habari wa manispaa ya Shinyanga ndugu Gaudiozi Mwombeki akikusanya kura,hapa ni katika awamu ya kwanza ya uchaguzi ambayo iliingiwa dosari baada ya baadhi ya wajumbe kukusanya kura zao kwa pamoja,hali ambayo ililalamikiwa na wajumbe wengine kwani ilikuwa na harufu ya uchakachuaji wa kura.Awamu ya pili(marudio) kila mjumbe alipiga kura peke yake na hatimaye mshindi akapatikana |
|
Tunasubiri matokeo yatangazwe........ |
|
Kufuatia uchaguzi huo wa kiti cha naibu meya,mshindi alitangazwa David Mathew Nkulila,diwani wa ccm kata ya Ndembezi,aliyekuwa anatetea kiti hicho,ambapo alipata kura 15,huku mgombea mwenza,George Mussa Kitalama(CHADEMA) akipata kura 6 |
Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga kwa awamu ya tatu sasa ndugu David Mathew Nkulila akizungumza baada ya ushindi wa kishindo ambapo aliwataka madiwani na wataalamu kuwajibika kama inavyotakiwa katika kuwaletea maendeleo wananchi,huku akiomba ushirikiano kwa madiwani na wataalam hao katika kuhakikisha kuwa ilani ya ccm inatekelezwa kama inavyotakiwa.
Naibu meya huyo alitumia fursa hiyo kuwataka watendaji/wataalam kutekeleza maazimio ya vikao vya baraza la madiwani kwa wakati unaotakiwa huku akisisitiza kuwa hataki kuona ufisadi wa aina yoyote katika manispaa hiyo
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin