TAZAMA PICHA_MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA DJ JUMA MIGETO MJINI SHINYANGA
Wednesday, July 16, 2014
Dj Juma Migeto enzi za Uhai wake
Mamia ya wakazi wa Shinyanga na maeneo jirani leo wamejitokeza kumzika Juma Migeto(32),ambaye enzi za uhai wake alikuwa DJ Maarufu kutoka Shinyanga,ambaye amefariki dunia juzi jijini Dar es salaam alipohamia kufanya kazi ya Udj.Mazishi yamefanyika mchana wa leo Jumatano katika makaburi ya Nguzo nane mjini Shinyanga.Pichani mwili wa marehemu ukitolewa katika msikiti wa MASJIDU THAQAFAL ISLAMIYAH,ulioko Majengo mjini Shinyanga,baada ya kuswaliwa
Enzi za uhai wake Dj Juma Migeto ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 32,akiwajibika
Kuelekea makaburini-Watu mbali mbali wenye mapenzi mema waliojitokeza kumsindikiza marehemu Juma Migeto kwenda katika nyumba yake ya milele katika makaburi ya Nguzo nane mjini Shinyanga
Kuelekea makaburini-Wakazi wa shinyanga wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Dj Migeto ,kipenzi cha watu
Katika barabara ya Nguzo nane mjini Shinyanga,mamia ya wananchi wakielekea makaburini.Dj Migeto alifariki dunia jijini Dar es salaam baada ya kuugua muda mrefu,ambapo inadaiwa kuwa alikuwa anahara na kutapika damu.
Enzi za uhai wake Juma Migeto alikuwa Dj mkali sana aliyetambulisha mkoa wa Shinyanga katika umahiri wake katika fani hiyo
Eneo la soko la Nguzo nane-Kuelekea makaburini
Ndivyo hali ilivyokuwa mchana wa leo mjini Shinyanga
Mwili wa marehemu unawasili makaburini-Ni katika makaburi ya Nguzo nane
Tayari mwili wa marehemu unafikishwa katika makaburi ya Nguzo nane kwa ajili ya mazishi mchana wa leo
Mwili wa marehemu Dj Migeto unaingizwa kaburini
Taratibu za mazishi zinaendelea
Watu mbalimbali waliohudhuria mazishi ya Juma Migeto
Ni katika eneo la makaburi ya Nguzo nane mjini Shinyanga
Mazishi yanaendelea
Karibu na kaburi la Juma Migeto
Mazishi yanaendelea
Mazishi yanaendelea
Mazishi yanaendelea
Mazishi yanaendelea
Baada ya mazishi,kaburi linamwagiwa maji
Katikati ni ustadhi Mwalimu Mbukuzi kutoka msikiti wa MASJIDU THAQAFAL ISLAMIYAH,ulioko Majengo mjini Shinyanga akitoa nasaha baada ya mazishi ya Juma Migeto ambapo pamoja na mambo mengine aliitaka jamii kuheshimu makaburi kwa kuepuka kuzungumzia mambo ya dunia wanapokuwa katika maeneo hayo,hivyo kuwataka kuzungumzia mambo yanayohusiana na msiba kwani sasa kuna tabia kwa baadhi ya watu wamekuwa wakicheka cheka makaburini badala ya kufuata kilichowapeleka
Baada ya mazishi
Baada ya mazishi,madj kutoka Shinyanga wakiwa mbele ya kaburi la marehemu Juma Migeto.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin