Waombolezaji nchini Ufilipino walipatwa na mshituko, pale mtoto wa miaka mitatu aliyekuwa "amekufa" kuzinduka wakati wanampeleka mazikoni.
Kwa mujibu wa gazeti la Metro -mtoto huyo kutoka Aurora, Zamboanga del Sur, alitangazwa kufa siku ya Ijumaa, na maziko kupangwa Jumamosi mchana.
Lakini wakati wa shughuli ya msiba, ndugu na marafiki walishtushwa wakati mtoto huyo "alipofufuka".
Watu walianza kurekodi tukio hilo baada ya padre aliyekuwa akifanya misa kugundua kuwa mtoto huyo amejisogeza, kabla ya kufungua macho.
Social Plugin