Waandishi mkoa wa Geita wakiwa na viongozi wa tume ya taifa ya uchaguzi,walipokutana mkoani Geita kuwapa mafunzo kuhusu mfumo wa matumizi ya Teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration(BVR).Wa kwanza aliyevaa suti nyeusi kutoka kulia ni mwandishi wa Malunde1 mkoani Geita blog Victor Bariety
Tume ya Taifa ya uchaguzi(NEC),imedai mfumo wa matumizi ya Teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration(BVR)uliotangazwa hivi karibuni,utatumika kwa ajili ya kuandikisha wapiga kura na sio kwa ajili ya upigaji kura kielekroniki(E-Voting) au vinginevyo.
Akizungumza juzi kwenye semina iliyokutanisha waandishi wa habari mkoani Geita wakati wa semina kuhusu mfumo huo mpya,Kamishina wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mchanga Mjaka alisema matatizo ya kuhesabu kura yaliyowahi kujitokeza katika nchi zilizowahi kutumia mfumo huo wa BVR hayatajitokeza kwenye zoezi la kuhesabu kura katika kura ya maoni ya Katiba Mpya na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Mfumo kama huo uliwahi kutumika katika nchi mbalimbali za Nigeria 2007,Ghana 2009,Liberia 2005,Guinea 2005,Mali 2005,Uganda 2008,Kenya 2013,Zambia 2008,Afrika Kusini na Zanzibar 2009.ambapo kuripotiwa kushindwa kukamilisha shughuli hiyo kutokana na sababu mbalimbali za kiufundi au ukosefu wa nishati ya umeme.
Kamishina huyo alisema changamoto zilizojitokea katika nchi hizo hazitajitokeza Tanzania kutokana na mfumo huo kutumika tu kwa ajili ya kujiandikisha na si upigaji wa kura na kuhesabu.
Alisema nchi hizo zilikwama katika hatua mbalimbali za uchaguzi kutokana na kutumia mfumo huo hata kwenye zoezi la upigaji na kuhesabu kura na kwamba uamzi wa kutumia mfumo wa BVR Umefikiwa kutokana na changamoto zilizojitokeza katika matumizi ya Teknolojia ya Optical Mark Recognition(OMR).
Alisema tayari vifaa vichache kwa ajili ya mafunzo ya vinategemewa kupokelewa wakati wowote Mwezi Julai Mwaka huu ili kuweza kutoa mafunzo kwa watendaji mapema na kwamba zoezi la uandikishaji litafanyika mwezi Agosti mwaka huu kwa siku 14.
Na Victor Bariety-Malunde1 blog Geita
Social Plugin