Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi Stadi (Veta) imevumbua boti inayojiendesha bila nahodha ambayo ina uwezo wa kutuma taarifa za kijasusi na kujilinda dhidi ya mashambulizi au uharibifu unaoweza kufanywa na watu wenye nia mbaya.
Akizungumza wakati wa Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini hapa jana, Mvumbuzi wa mashine hiyo, Immanuel Bukuku alisema kuwa imemchukua miezi sita kufanikisha uundaji wa mashine hiyo.
Alisema uvumbuzi huo umeambatana na majaribio ambayo yamefanyika katika Pwani ya Kigamboni na yameonyesha mafanikio makubwa na ipo tayari kwa ajili ya matumizi ikiwa na kamera za kutosha kwa ajili ya uchunguzi na kupeleka taarifa.
alisema na kuongeza kuwa boti hiyo itakuwa inaongozwa na mashine nyingine itakayo kuwa sehemu maalumu.
Bukuku ambaye ni mwalimu wa masuala ya Sayansi na Teknolojia katika Chuo cha Veta Chang’ombe alisema amevumbua boti hiyo ambayo imetengenezwa kwa kutumia vifaa rafiki na mazingira ya bahari na inatumia mfumo wa umeme jua na mashine za kuzalisha umeme.
alisema.
Alisema pia amefanikiwa kutengeneza injini ya ndege ambayo imeonyesha mafanikio kwa kiasi kikubwa na wakati wowote inaweza kutumika na mafanikio hayo yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mpango wa Veta wa kuwa na Kitengo cha Masuala ya Ufundi na Ubunifu.
alisema na kuongeza kuwa kitengo hicho kimepania kubadili mwelekeo mzima wa Veta kwa hivi sasa.
Social Plugin