Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UNESCO NA KOICA ZASAIDIA MAISHA ENDELEVU USAMBARA MASHARIKI

Hapa ni  katika wilaya ya Mukinga mkoani Tanga-Picha na  Myoung Su Ko 

Dar es Salaam Julai 11, 2014.
Jamii zinazoishi katika Hifadhi Bioanuwai ya Milima ya Usambara Mashariki zinatarajiwa kukuza uwezo wao wa kutumia rasilimali zao za asili kwa njia endelevu. 

Kupitia mradi wa UNESCO wa Shilingi za Tanzania milioni 700, “Uchumi wa Kijani katika Hifadhi Bioanuwai (GEBR) unaofadhiliwa na KOICA (Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea), wananchi watapunguza utegemezi wao wa kiuchumi kwa kukata miti. 

Baadhi ya shughuli za mradi huo kwa ajili ya kujenga uwezo zinahusisha mafunzo ya aina tatu kwa jamii kuhusu Biashara ya Kijani katika Bioanuwai ya Milima ya Usambara Mashariki huko Tanga. 

Mafunzo ya kwanza yanatarajiwa kufanyika Julai 2014. 

Mafunzo hayo yataandaliwa na EUBR kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii. 

Jamii watapewa mafunzo juu ya usimamizi wa biashara, masoko, uhasibu, fedha, ujasiriamali, na elimu ya mazingira na bioanuai. 

Jamii zitakazopata mafunzo zitaongeza uelewa wao juu ya umuhimu wa kuunganisha masuala ya biashara na mazingira na kuanzisha akili ya ujasiriamali ambayo itasababisha upanuzi wa biashara za kijani zilizopo na kujenga nyingine mpya. 

Mafunzo mengine mawili yatafanyika mwishoni mwa mwaka huu na mazingira tofauti, lakini ni kuhusiana na kuanzishwa kwa biashara ya kijani.

Mjasiriamali wa biashara endelevu, Jason J Drew alisema

 ‘Hapo awali watu waliongelea mikataba ya kibiashara inayoleta faida kwa pande zote mbili, walikuwa wapuuzi, daima mazingira yalikuwa ndio yanayoshindwa.'

 UNESCO inatumaini kupitia mradi huu kwamba uasili wa kipekee, wa ajabu na wa kuvutia wa Tanzania hautashindwa.

Hata hivyo, katika mikutano ya kupanga na kushauriana iliyofanywana EUBR katika ngazi ya jamii Machi 2014, maoni ya pamoja yaliyowekwa kwa muhtasari na wadau katika kuelekea kwenye Biashara ya kijani kwa ajili ya kulinda viumbe hai ili kuongeza kipato bila kuharibu mazingira'.

Karibu asilimia 38 ya ardhi ya Tanzania ni misitu na sehemu tambarare, na ni pamoja na mazingira muhimu ya asili na makazi ya wanyamapori.

 Zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania wanaishi katika maeneo ya vijijini ambao hutegemea sana maliasili na kilimo.
 Hali hii imekuwa kikwazo kwa kuhifadhi misitu kutoka kwa shughuli za kiuchumi za binadamu.

 Ili kurekebisha hali hii, Mpango wa UNESCO wa Binadamu na Hifadhi Hai (MAB) wa (1971) umekuwa ukiunganisha binadamu na uasili badala ya kutenganisha viwili hivyo na miradi mbalimbali ya ndani na nje ya hifadhi hai ambayo imesababisha maendeleo endelevu.

Nchini Tanzania, Hifadhi Hai ya Usambara Mashariki mkoani Tanga iliteuliwa kama moja yaH ifadhi Hai mwaka 2000, baada ya Hifadhi Hai nyingine mbili, Serengeti-Ngorongoro (1981) na Ziwa Manyara (1981).

 Kanda ya Usambara Mashariki ni walengwa wa mradi wa GEBR, na unashughulikia maeneo yanayozunguka wilaya za Muheza, Mkinga, na Korogwe.

Kutakuwepo na mafunzo kwa wananchi kuhusu usimamizi wa biashara, masoko, uhasibu, fedha, ujasiriamali, na elimu ya mazingira na bioanuai kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 24 huko MkoaniTanga.

 Mafunzo ya kwanza yatafanyika kijiji cha Mnyuzi, Tanga nawaandishi wanakaribishwa kuripoti.


 Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
UNESCO Ofisi ya Dar es Salaam (dar-es-salaam@unesco.org)
P.O. Box 31473
127 C, Mtaawa Mafinga (Kando kando ya Barabara ya Kinodoni) Dar es Salaam Tanzania
Simu: +255-22-266 6623 Nukushi: +255-22-266 6927.  Mobile:Stella Vuzo 0767100 902

Na majarida ya UNESCO kuhusu mradi wa GEBR:
http://www.unesco.org/new/fileadmin/MULTIMEDIA/HQ/SC/pdf/MAB_national_report_ROK_MABICC25_en.pdf



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com