Dj Migeto enzi za uhai wake Mwili wa marehemu Juma Migeto tayari umesili mjini Shinyanga kutoka Jijini Dar es salaam kwa ajili ya mazishi mchana huu |
Juma Migeto alifariki dunia juzi majira ya saa tano asubuhi wakati akipata matibabu katika hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Mazishi yanatarajia kufanyika mchana huu leo Jumatano saa saba mchana katika makaburi ya Majengo mjini Shinyanga.
Hivi sasa msiba wa marehemu Juma Migeto upo nyumbani kwao eneo la Kambarage karibu kabisa na uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Juma Migeto,mzaliwa wa Shinyanga alikuwa anajishughulisha na kazi ya U Dj mkoani Shinyanga na baadaye kuhamia jijini Dar es salaam akiendeleza kazi yake ya U dj katika maeneo mbalimbali jijini humo.
Taarifa zaidi utaendelea kuzipata kupitia blog hii ya Malunde1 blog,Fahari ya Shinyanga
Social Plugin