Hapakuwa na kiingilio,African Barrick waliwezesha mpanga mzima-Pichani ni Wakazi wa Kahama wakiwa katika uwanja wa taifa usiku wa kuamkia leo wakati mechi ya fainali kati ya Argentina na Ujerumani zikiumana vikali nchini Brazili.Wakazi hao wa Kahama mbali na Kushuhudia mechi za kombe la dunia pia walipata fursa ya kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwemo Ney wa Mitego,Christaina Bella na wasanii kutoka Kahama
Msanii Ney wa Mitego akiwakuna wakazi wa Kahama usiku wa kuamkia leo mjini Kahama,African Barrick Gold ndiyo waliofadhili mpango mzima,ikiwa ni katika kuimarisha uhusiano wao na jamii inayowazunguka,lakini kuonesha kuwa migodi ni kwa manufaa ya wananchi
Wimbo wa Ney wa Mitego ukaibua hisia_Maisha menyewe mafupi.........
Ney anakamuaaaa_Burudani kwa wakazi wa Kahama ilikuja muda mfupi baada ya kumalizika kwa Soka Bonanza ambapo jumla ya timu 8 za mpira wa miguu kutoka Kahama zilikuwa zinashiriki mashindano hayo.Mshindi wa kwanza alikuwa Bodaboda fc,akifuatiwa na Afya fc ambao waliingia fainali kama ilivyokuwa katika kombe la Dunia Argentina na Ujerumani huko Brazil
Ebwana eee,ilikuwa burudani sana,hayo yote ni kwa sababu ya uwepo wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold inayomiliki mgodi wa Buzwagi na Bulyanhulu wilayani Kahama,lakini Brazuka Bonanza mjini Kahama ilikuwa inasimamiwa na mgodi wa Buzwagi
Mwenye nguo nyeupe ni msanii matata kutoka Kahama anajulikana kwa jina la Joslin Abraham akichana mistari mbele ya Ney wa Mitego.Mbali na msanii huyo kutoka Kahama kuonesha kipaji chake cha kuimba pia wasanii wengi wa Kahama walipanda jukwaani na kufanya mambo makubwa,hakika ilikuwa full shangwe,tena bila pesa,wengi wakisema "Asante Buzwagi"
Msanii Christian Bella akishambulia jukwaa katika uwanja wa taifa Kahama usiku wa kuamkia leo ambapo maelfu ya wakazi wa Kahama walikuwepo katika uwanja huo
Msanii Christian Bella akifanya yake mjini Kahama.Mbali na kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali walioletwa na African Barrick,wakazi wa Kahama walishuhudia live mechi ngumu kati ya Argentina na Ujerumani,hakuna aliyelala mpaka kikaeleweka Ujerumani 1,Argentina 0.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Social Plugin