MLEMAVU AKATAZWA KUENDESHA GARI,HANA MIKONO LAKINI ANAENDESHA GARI
Sunday, July 06, 2014
Polisi nchini China wamemkamata mtu asiyekuwa na mikono akiendesha gari. Bwana huyo Wo Guo (45) si tu kwamba hakuwa na leseni bali alikuwa akitumia mguu wake wa kulia kubadili gia huku mguu wa kushoto ukikanyaga mafuta na breki.
Msemaji wa polisi amesema:
Ni jambo la ajabu, lakini ni hatari sana kwake kuendesha gari.
Polisi huyo amesema itakuwa vyema kama ataajiri dereva wa kumuendesha. Gari la bwana Wo linashikiliwa na polisi ili kumzuia asiendelee kuendesha.
Social Plugin