Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAFANYABIASHARA GEITA WATOA PIKIPIKI 40 KUPAMBANA NA WAHALIFU

WANANCHI wa Mkoa wa Geita wametakiwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ili kuhakikisha wanaoingia mkoani humo wanakamatwa kabla hawajafanya uhalifu wa kuiba na kuwauwa vikongwe jambo ambalo limekithiri katika Mkoa wa Geita.
 
Kauli hiyo imetolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Geita Said Magalula wakati wa kupokea pikipiki 40 na mafuta ya petroli lita 1000,  baiskeli 4 zilizotolewa na wafanya bishara Mkoa humo kwa ajili ya kupambana na wahalifu wanaoingia kwa ajili ya kufanya uhalifu zoezi lilfanyika katika ukumbi wa bwalo la polisi lililoko mjini Geita.
 
Saidi alisema kuwa wananchi wa mkoa huo kuanzi Kata, Vijiji na Vitongoji na tarafa  wanatakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa  jeshi hilo hili waweze kupambana na wahalifu kwa kutumia vifaa walivyo pewa na wafanya bishara hao waliojitoa kwa moyo wa dhati na kumtaka kamanda wa jeshi hilo kutunza vyombo hivyo kwa makini kuhakikisha vinafanya kazi zilizo kusudia na sio vinginevyo.
 
Naye Mwenyekiti wa wafanyabiashara Leonard Bugomola alisema kuwa wamemua kutoa pikipiki 40 na mafuta ya Petroli lita 1000, baiskeli 4 kutokana na umakini wa kuwa kamata majambazi wawili walifanya tukio la mauaji la kumua mfanyabishara mwenzao hivi karibuni wakati akiwa dukani kwake.
 
Amesema wao kama wafanyabishara wa Mkoa watahakikisha wanaendea kulisaidia jeshi hilo kwa vifaa mbalimbali na kuyataka mashirika na watu binafsi wenye moyo wa kuendelea kulisaidia jeshi hilo  ili ulinzi uzidi kuwa imara na wakutosha na wahalifu wanaoingia kwa ajili ya uhalifu washindwe kutoka.
 
Naye Kamanda wa Mkoa wa Geita Joseph Konyo alishukuru wafanya biashara hao kwa kujitoa kwa moyo na kuwaomba wananchi wote wa Mkoa kuendelea kutoa msaada hata kama siyo fedha chochote kitauzwa ili pesa zipatikane kwa ajili ya kuimalisha ulinzi katika Mkoa huu.
 
Namshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kukubali kuwa mgeni rasmi na ninyi wafanya bishara nawashukuru sana nawaomba tushirikiane kwa pamoja ili kuimarisha ulinzi kwa kutoa ulicho nacho si lazima fedha na yeyote anayefikiria kuiba Geita sasa hivi kuna ulinzi wa kutosha alisema Konyo

Na Valence Robert-Malunde1 blog Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com