Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO WAPIGWA MARUFUKU MJINI KAHAMA

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya
 
Wafanyabiashara wadogowadogo waliopo kwenye masoko yasiyo rasmi katika Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga, wametakiwa kuondoka mara moja kabla hawajafikiwa na Oporesheni ya kuwaondoa kwa nguvu inayoendelea katika Halmashauri hiyo.

Hauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya wakati akiongea na wafanyabiashara wa soko jipya la Mayila lililopo Kata ya Nyihogo ambapo amedai serikali haina utaratibu wa kila mtu kuanzisha soko anavyotaka. 

Mpesya amewataka wananchi kumpa orodha ya masoko yasiyo rasmi ikiwemo soko la kwa Mlapa lililopo kati ya Kata za Mhungula na Nyihogo, ambalo walishaondolewa na kuanza kurudi, na kwamba watakaokamatwa watachukuliwa hatua za kisheria. 

Awali Wafanyabiashara hao walimueleza Mpesya kuwa wanashindwa kulipa ushuru katika Halmashauri ya Mji kutokana na biashara zao kuathiriwa na uanzishwaji wa masoko holela mitaani hali ambayo Mpesya amesema wahusika watakumbwa na oporesheni hiyo inayoshirikisha Jeshi la Polisi. 

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nyihogo Amosi Sipemba amesema wafanyabiashara hao wamewekeza zaidi ya Shilingi Bilioni Tatu katika soko la mayila ili serikali iweze kunufaika ni lazima masoko ya mitaani yaondolewe.

Akizungumzia soko la Wakulima Mpesya amesema Wafanyabiashara katika eneo hilo lazima waondoke baada ya kukamilika kwa soko la Majengo kwakuwa eneo hilo Serikali hainufaiki na chochote wakati ikitumia gharama kubwa kusomba taka za soko hilo. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com