UTAPELI sasa wachukua sura mpya mkoani Iringa bada ya baadhi ya waganga wa tiba asilia (Sangoma) kugeuziana kibao wenyewe kwa wenyewe kwa kuanza kufanyiana utapeli wa kutisha ikiwa ni pamoja na kujifanya maofisa wa polisi na kuwatapeli fedha wenzao zaidi ya 60.
Imedaiwa kuwa waganga hao matapeli wana mtandao wao na wamekuwa wakiwatumia askari wasio na maadili ya jeshi la polisi kwa kwenda kuwatisha waganga wachanga kwa madai kuwa wao ni maofisa wa polisi na serikali ambao wanafuatilia leseni zao za kazi na kuwatisha kuwa wanafanya kazi kienyeji hivyo wanapaswa kufikishwa polisi na wakiwa njiani wanawataka kutoa rushwa kati ya 300,000 hadi milioni moja ama kuingia nao makubaliano ya mkopo ya fedha hizo za rushwa kabla ya kuwaachia.
Katibu wa chama cha wanganga wa tiba asilia wilaya ya Iringa Dr Salum Kalolo (pichani) alithibitisha jana kuwepo kwa utapeli huo na kuwatayari chama chake kimeanza kuchukua hatua ya kuwasaka matapeli hao ambao tayari baadhi yao majina yao yanafahamika na wanaendelea kusakwa ili kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Dr Kalolo alisema kuwa awali utapeli huo ulikuwa ukifanyika chini kwa chini na ili kuwa ni siri ila kwa sasa utapeli huo umeendelea kufanyika wazi wazi na tayari kama chama kimeona ni tatizo kubwa ina iwapo watanyamaza kimya madhara yanaweza kuwa makubwa zaidi .
" Tunasikitika sana kuona kuwa waganga wa tiba asilia wameacha kufanya kazi yao ya uganga na wamejiingiza katika wimbi la utapeli wa kuwatapeli wanganga wenzao fedha kwa kutumia njia ya vitisho mbali mbali.....tena mbaya zaidi wanawatumia baadhi ya askari kufanya utapeli huo"
Alisema kuwa waganga hao matapeli wamekuwa wakijipachika vyeo mbali mbali zikiwemo vya polisi na maofisa wa serikali kupitia wizara ya afya kwa madai wametoka makao makuu na wapo mkoani hapa kwa ajili ya kufanya ukaguzi mbali mbali kwa waganga wa tiba asilia jambo ambalo si kweli bali wamelenga kujipatia fedha kwa njhia ya udanganyifu
Dr Kalolo alisema kuwa tayari waganga zaidi ya 60 wametapeliwa katika Manispaa ya Iringa , Kilolo ,Iringa vijijini na wilaya ya Mufindi na kuwa wao kama chama wamekwisha wakamata baadhi ya wanganga hao na pindi wanapowafikisha polisi wamekuwa wakiachiwa huru .
Hivyo ameliomba jeshi la polisi na serikali ya wilaya na mkoa kusaidia kukomesha utapeli huo ili kuepusha madhara zaidi kujitokeza mkoani Iringa.
Mbali ya kuomba jeshi la polisi na serikali kusaidia kukomesha tabia hiyo pia alisema hatua ambayo chama chake kimechukua ni pamoja na kuendesha zoezi la kuyaondoa barabarani na mitaani mabango yote ambayo yamewekwa na waganga hao wasio fahamika .
Wakati huo huo chama hicho cha wanganga wa tiba asilia wilaya ya Iringa kimeiomba serikali kuangalia uwezekano wa kutenga bajeti kifedha kwa ajili ya wanganga hao kupitia vyama vyao ili kuendelea kuboresha zaidi huduma yao .
.
Kwani alisema huduma ambazo wanganga hao wanazitoa ni kwawananchi wa Tanzania hivyo kama ilivyo katika sekta ya afya ambazo zimekuwa zimekuwa zikitengewa bajeti.
Na Francis Godwin blog Iringa
Social Plugin